Home Habari za michezo KRAMO NNJE TENA SIMBA….AL AHLY WAINGIZA MASTAA WAPYA MECHI YA KESHO….

KRAMO NNJE TENA SIMBA….AL AHLY WAINGIZA MASTAA WAPYA MECHI YA KESHO….

Habari za Simba

Mlinda mlango wa wa klabu ya Simba Sc, Aishi Manula ‘Air Manula’ na winga Aubin Kramo hawatakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitakipiga kwenye mchezo wa marudiano wa michuano ya African Football League dhidi ya Miamba ya Misri na Afrika Al Ahly.

Manula ameshapona majeraha yake lakini hayupo fiti kimchezo japo kuwa ameshaanza mazoezi na wachezaji wenzake huku Kramo bado yupo nchini kwao ambapo alienda kuuguza majeraha yake yaliyokuwa yanamsumbua.

Kwenye orodha ya wachezaji 24 waliosafiri kuelekea nchini Misri majina ya Aishi Manula na Aubin Kramo hayapo hii inaashiria kutokuwepo kabisa kwenye mchezo huo unaotarajiwa kupigwa Oktoba 24 katika dimba la Cairo International.

Wakati huo huo, Klabu ya Al-Ahly imethibitisha kuwa Mlinzi wao wa kushoto mwenye magoli 50 katika klabu hiyo Ali Maaloul aliyeukosa mchezo wa Dar wa michuano ya AFL amerejea kwenye kikosi hicho Kuelekea mechi ya marudiano ya AFL dhidi ya Simba huko Misri.

Pia klabu hiyo imethibitisha kuwa Emam Ashour nae atakuwa seheme ya wachezaji watakaoitumikia klab hiyo kwenye mchezo huo ujao wa AFL,

Vilevile mshambuliaji wao mpya ambaye amewahi kucheza ligi kuu ya Ufaransa na Ujerumani Anthony Modeste ambaye hakuweza kusafiri na wenzake kwenda nao Dar es Salaam kwenye mchezo wa awali wa AFL dhidi ya Simba Kutokana na Masuala ya Kiafya kwa upande wake, nae amerejea kwenye kikosi Kuelekea mechi hiyo

SOMA NA HII  MZEE DALALI:- MGUNDA ANA OFA NYINGI ZA KWENDA ULAYA....ANAWEZA KWENDA MAN UNITED...