Home Habari za michezo MZEE DALALI:- MGUNDA ANA OFA NYINGI ZA KWENDA ULAYA….ANAWEZA KWENDA MAN UNITED…

MZEE DALALI:- MGUNDA ANA OFA NYINGI ZA KWENDA ULAYA….ANAWEZA KWENDA MAN UNITED…

Habari za Simba leo

Mjumbe wa Bodi ya Simba, Mzee Hassan Dalali amesema kuwa Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Juma Mgunda ni kocha bora na anafaa kuaminiwa na uongozi wa timu hiyo moja kwa moja.

Dalali amesema hayo baada ya Mgunda kuiongoza Simba katika mechi 4 na kufanikiwa kushinda mechi 3 na sare moja huku timu yake ikiwa imefunga mabao 9 na kuruhusu bao 1.

“Utashangaa Juma Mgunda kufundisha Simba, si ndiyo timu yake? Kwani alifukuzwa? Mgunda yupo. Kwanza bonge la kocha na soka analijua, amefanya mambo makubwa sana kwenye soka la Tanzania, amecheza soka kwa kiwango cha juu mpaka Timu ya Taifa na alikuwa anafunga mabao.

“Mgunda ana leseni A, anaweza kufundisha hata Manchester United, Chelsea uwezo anao na leseni anayo. Mgunda ana ofa kibao Ulaya lakini ameambiwa kaa hapa hapa Simba na ana uchungu nah ii timu.

“Mgunda falsafa yao ni vijana wadogo, ndio anawatumia. Duchu kafunga bao la tatu mpaka amelia kwa uchungu pale chini. Vijana wapewe nafasi na makocha wazawa waaminiwe, sio mtu analipwa mamilioni lakini wapi?” amesema Mzee Dalali.

SOMA NA HII  KANOUTE AFUATA NYAYO ZA CHAMA...NAE ASEPA SIMBA