Home Habari za michezo ROBERTINHO ATAMBA AWAPA NENO HILI MASHABIKI

ROBERTINHO ATAMBA AWAPA NENO HILI MASHABIKI

Tetesi za Usajili Simba

Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kuwa timu yake ina kikosi kipana hivyo imemsaidia yeye kufanya mabadiliko na kupata ushindi pale anapotaka.

Robertinho amesema hayo jana baada ya ushindi wa Simba wa bao 2-1 dhidi ya Singida Fountain Gate FC, katika FDimba la Liti.

“Sikia, nafikia ilikua ni mechi ngumu lakini, kipindi cha kwanza kilikua bora, tuna wachezaji wenye vipaji. Lakini, sikia, kipindi cha pili nafikiri, maamuzi yetu yalikua bora, kwa sababu nilitoa nafasi kwa baadhi ya wachezaji.

“Unajua kuhusu hilo ninafuraha nalo lakini, wachezaji wangu, wachezaji wa idara ya viungo wanafanya vitu vingi kuisaidia timu kushinda. Malengo ya Simba ni kucheza vizuri na kushinda, pointi tatu ni muhimu zaidi, mpango wetu ulikua ni ushindi.

“Kwenye mechi mbili na tuna kikosi kipana, Simba si timu ndogo, ni timu kubwa, pongezi nyingi kwa mashabiki wetu,” amesema Robertinho.

SOMA NA HII  RIVERS UNITED WAZIDIWA KETE NA YANGA...WACHACHAWA! WAPAGAWA!...ISHU NZIMA IKO HIVI