Home Habari za michezo WAKATI LEO NI ROUND YA PILI YA AFL…SIMBA WAFUNIKA TIMU ZOTE KWA...

WAKATI LEO NI ROUND YA PILI YA AFL…SIMBA WAFUNIKA TIMU ZOTE KWA TAKWIMU….

Habari za Michezo

Ni wiki nyingine kwa wapenzi wa soka Africa, kuendelea kushuhudia radha ya soka katika mashindano ya AFL baada ya kutamatika kwa mzunguko wa kwanza(The first leg round).

Hakika mzunguko wa kwanza ulikua ni bora sana, wenye mengi ya kuvutia bila kusahau kero za hapa na pale. Nitatoa baadhi ya mifano, tukio lenye kuvutia lilihusisha mechi ya Simba vs Al Ahly, Damn…The game was so good. Mechi iliyopambwa na sherehe za ufunguzi. Ijumaa ilikuwa bora sana.

Tukio kubwa la kukera na lililoleta taswira mbaya katika mashindano basi ni la mchezaji wa Enyimba, Innocent (3) kuandika jina lake kwa kutumia kitu chenye mfano wa chokaa nyeupe au pen, inachekesha
, lakini hii ni aibu kwa Enyimba na Nigeria kwa ujumla.

Turudi kwenye mechi sasa, Simba Sports Club imeonesha kuwa na takwimu bora, sijasema matokeo, TAKWIMU bora zaidi katika mashindano hayo. Narudia tena, Takwimu sio matokeo pekee.

Katika list hii nitaweka takwimu zenye umuhimu zaidi kama vile idadi ya magoli, Shot on Target, Complete Passes na ufanisi wa pasi(Pass Accuracy).

1. SIMBA SPORTS CLUB.
Complete passes – 546
Pass accuracy – 86%
Shot on Target – 6
Goals- 2

2. MAMELODI SUNDOWNS
Compete passes- 479
Pass Accuracy- 70%
Shot on Target – 3
Goals – 2

3. AL AHLY
Complete Passes- 390
Pass Accuracy – 78%
Shot on Target – 4
Goals – 2

4. ES TUNIS
Complete Passes- 481
Pass Accuracy – 79%
Shot on Goal – 2
Goals – 0

Na list inaendelea, hizo timu zilizobaki namba zao ni au chini ya nne; upande wa on Target, Chini ya 400 passes huku pass accuracy ni chini ya 75% bila kusahau walio score ni goal moja moja. Huku timu nyingine zikitoka bila goal la kufutia machozi.

Ikikumbukwe, nimeangalia mechi zote ila bado mechi iliyoonesha radha na mvuto zaidi basi ni ile mechi ya ufunguzi kati ya Simba na Al Ahly.

Ukitoa kuwa ni mechi ya ufunguzi, ila ni mechi iliyo amsha radha ya AFL huku wengi kutoka mataifa ya Africa(ukitoa Tanzania) wamefurahishwa na performance ya Simba ambaye walihisi ni Underdog katika mechi yenye tukio kubwa kama lile, ila walishangaa ilijitahidi kuonesha maturity ya hali ya juu hata pale baada ya mpinzani wake kupata magoli.

Pia, hata wachezaji wengi wa Timu zinazo shiriki walifanya hii mechi kama ni mzani wa performance zao katika AFL, mfano Nahodha wa ES TUNIS alinukuliwa katika mahojiano akisema, anatamani na watajitahidi mechi yao iwe bora na yenye ushindani kama ile ya Simba Vs Al Ahly. Unaweza ona kwa namna gani mechi iliyokuwa bora.

N.B. Kuna kelele huku mtaani kusema Simba alikuwa afungwe zaidi ya goli tano. Ni kweli kuna clear chance Al Ahly wamekosa, ila kuna mwanadada nampenda alisema “Almost doesn’t count” akimaanisha nearly doing something is not the same as actually doing it.
Sawa leo Yanga aje aseme ilibaki kidogo tu nishiriki AFL, why? Sababu …..I don’t know, Karia alituombea na sisi tushiriki. Jokes.

Simba inachangamoto zake, Simba inawezatolewa katika mashindano haya, lakini hii haifuti ubora wake aliou-onesha katika huu mzunguko wa Kwanza.

CREDIT: JAMII FORUM

SOMA NA HII  AMBOKILE APEWA MWEZI MMOJA NKANA