Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said amesema Klabu ya Yanga inastahili kuwa miongoni mwa vilabu 10 Bora vya Afrika kwa sasa kutokana na mafanikio makubwa ambayo wameyapata.
Shirikisho la Soka barani Afrika limeitaja klabu ya Yanga kuwa miongoni mwa timu 10 zinazowania tuzo ya klabu bora Afrika kwa mwaka 2023.
Yanga SC itachuana na Marumo Gallants, USM Alger, CR Belouizdad, Al Ahly, Raja CA, Wydad AC, Mamelodi Sundowns, Asec Mimosas na ES Tunis katika kinyang’anyiro hicho. Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Desemba 11, 2023 Jijini Marrakesh nchini Morocco.
“Klabu ya Yanga ya Tanzania ni miongoni mwa klabu 10 Bora Afrika zinazogombea Klabu Bora Afrika kwa mwaka kwa msimu wa 2022-2023.
“Yanga waliocheza fainali ya Kombe la Shirikisho la AFRIKA ndiyo klabu pekee kutoka Tanzania na ukanda wa CECAFA.”
“Sidhani kama kuna mtu ana shaka na jambo hili, kwa walichokifanya Yanga msimu uliopita wanastahili kuwemo humu, nadhani hata Simba hawatosema ila wakikaa peke yao watasema… “Wanastahili mabwege wale ila tutakoma.”
“Hongera sana klabu ya marehemu baba yangu Mzee Said Kazumari Mtipa. You deserve all this for you had a very good season 2022/2023,” amesema Jemedari Saidi.