Uncategorized

YANGA YAPANIA KUIFANYA SIKU YA WANANCHI YA KIPEKEE ZAIDI

admin July 25, 2019 6:36 am

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umejipanga kuifanya siku ya wananchi kuwa ya kipekee kuliko zote kutokana na ukubwa Yanga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ndani ya Yanga, Deo Muta, amesema kuwa ni wakati wa mashabiki kuipa sapoti timu ya Yanga na kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa.

“Tumejipanga kuifanya iwe siku ya kipekee na wiki yenyewe itakuwa na matukio mengi ya kijamii hivyo ni fursa ya mashabiki kujitokeza kwa wingi.

“Tutakwenda Zanzibar ambapo ni sehemu ya muungano wa Tanzania lengo ni kuifanya iwe siku ya tofauti,” amesema.

Kilele cha siku ya wananchi itakuwa Agosti 4 uwanja wa Taifa ambapo Yanga iacheza na Kariobang Sharks mchezo wa kirafiki.

NYOTA MPYA WA MTIBWA AANZA NA MAKEKE YAKUTOSHA BARCELONA YATOA LISTI YA WACHEZAJI SITA KWA PSG KUMPATA NEYMAR JR

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply