Home Habari za michezo ROBERTINHO ACHIMWA MKWARA MZITO…… KINACHOFANYIKA KWENYE DABI NI ZAIDI YA AFL

ROBERTINHO ACHIMWA MKWARA MZITO…… KINACHOFANYIKA KWENYE DABI NI ZAIDI YA AFL

Habari za Simba

WAKIJIANDAA na mchezo wao wa Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu wa Simba, Robert Olivieira ‘Robertinho’ amechimba mkwara mzito kuwa wametumia uzito wa michezo yao miwili ya AFL, dhidi ya Al Ahly kujiandaa na uzito wa mchezo wa Jumapili huku akitenga siku tano sawa na saa 120 kujiandaa na mchezo huo.

Kikosi cha Simba jana Jumanne kilianza rasmi kambu ya maandalizi ya mchezo huo wa Jumapili dhidi ya Yanga ambapo Simba watakuwa wenyeji mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba wanaingia katika mchezo huu wakiwa wamecheza mchezo mmoja tu, wa Ligi Kuu Bara baada ya kutoka kwenye ratiba ya mashindano ya African Football League ambayo waliishia robo fainali baada ya matokeo ya jumla ya sare ya mabao 3-3.

Akizungumza na Championi Jumatano, Robertinho alisema: “Ni kweli tunatarajia mchezo mgumu sana mbele ya Yanga kutokana na ubora wa kikosi chao, lakini kama kikosi tunajivunia ubora wa maandalizi yetu kuelekea mchezo huu.

“Tumekuwa na michezo miwili mikubwa dhidi ya Al Ahly ambayo naweza kusema tulicheza kwa ubora mkubwa na tunapaswa kucheza katika kiwango bora zaidi ya kile ili kuweza kupata ushindi mbele ya Yanga lakini pia tumeanza maandalizi mapema.”

SOMA NA HII  NYUMA YA PAZIA....HIVI NDIVYO MGUNDA ANAVYODILI NA KINA MKUDE NDANI YA SIMBA...NI KIMYA KIMYA YANI...