Habari za Simba
Habari za michezo

ROBERTINHO AUKUBALI MZIKI WA YANGA…… ASEMA HAYA

Staff Desk November 6, 2023 10:39 am

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewapongeza wapinzani wao wa jadi Yanga SC kwa kushinda dabi waliyoipiga jana Novemba 5, 2023 na kuibuka na ushindi wa 5-1.

Akizungumzia mchezo huo mara baada ya kumalizika kwa Simba kupoteza kwa kichapo hicho kizito, Robertinho amesema, wachezaji wake kipindi cha kwanza walicheza vizuri lakini kipindi cha pili walikuwa wanaacha nafasi kubwa kwa mpinzani.

“Walikaa nyuma sana na kutoa nafasi kwa mpinzani kufunga magoli mawili haraka lakini kimsingi niwaponmgeze wapinzani, wamecheza vizuri kipindi cha pili na kushinda dabi,” alisema Robertinho.

Yanga wamezidi kujikita kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 21 wakiwa wamecheza michezo nane huku Simba akishika nafasi ya tatu akibaki na alama zake 18 kwa michezo yake saba aliyocheza.

FEI TOTO HUKU AZAM NI MPYA KABISA JAPO USHINDI NI MNONO ILA UKWELI WA LIGI KUU UPO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply