Habari za michezo

YANGA BADO ANAMSAKA PACHA WA MAYELE

Staff Desk November 11, 2023 2:25 pm

Taarifa za uhakika kutoka Yanga SC ni kwamba klabu hiyo inaufuatilia kwa karibu uongozi wa mshambuliaji Sankara William Karamoko (20) ili kupata saini yake katika dirisha lijalo la usajili.

Sankara raia wa Ivory Coast anahitajika Yanga ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji katika klabu hiyo na tayari wanajiandaa kutuma ofa, ni mshambuliaji mzuri sana.

Yanga wamerejea kwenye mchakato wa kusaka huduma ya mchezaji huyo baada ya kumkosa katika usajili uliopita ambapo mambo kadhaa hayakwenda sawa.

Iwapo Yanga watafanikiwa kumpata Sankara basi watakuwa wamelamba dume na kutengeneza partnership nzuri kwenye safu ya kiungo na ushambuliaji hasa ikizingatiwa kuwa amecheza pamoja na Aziz Ki na Pacome Zouzoua katika kikosi cha ASEC Mimosas.

MOMO AWASHAURI VIONGOZI WA SIMBA, HERSI WA YANGA ATAJWA YANGA AMTAFUTIA MSAIDIZI KIUNGO MKABAJI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply