Habari za michezo

BANGO LA YANGA LAZUA MJADALA ACHAMBUZI ASEMA HAYA

Staff Desk November 15, 2023 11:49 am

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia Kipenga Extra ya East Africa Radio, Martin Mwakiposa amesema kuwa kitendo cha Klabu ya Yanga kuweka bango barabarani kuwazodoa wapinzani wao Simba Sc ni sahihi kwani ni sehemu ya kuwapa furaha mashabiki zao.

Mkunda amesema hayo baada ya Yanga kuweka bango barabarani linaloonyesha mabao 5-1 waliyowafunga wapinzani wao Simba, Novemba 5, 2023.

“Mimi siwalaumu Yanga kuweka lile bango, kwa sababu imepita takribani miaka 13 ndio tunaona tukio kama hili la mtu kufungwa goli 5. Kwa hiyo Yanga wanachofanya ni kuwafurahisha mashabiki zao.

“Na njia mojawapo ya kuwafurahisha ni kuweka bango ambalo atakayepita akiwa kwenye upande wa goli 5 itaendelea kutoa tabasamu, lakini atakayekuwa kwenye upande wa goli 1 itazidi kumkera,” amesema Martin Mwakiposa.

KWENYE HILI SIMBA WAKIAMUA YANGA HAWACHOMOKI BANGO LA YANGA LAIPELEKA SIMBA MAHAKAMANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply