Home Habari za michezo BAADA YA KUNASA SIRI ZOTE ZA WAALGERIA….GAMONDI KATIKISA KICHWA KISHA AKASEMA HILI…

BAADA YA KUNASA SIRI ZOTE ZA WAALGERIA….GAMONDI KATIKISA KICHWA KISHA AKASEMA HILI…

Habari za Yanga SC

Kocha mkuu wa Yanga , Miguel Gamondi amefunguka kuwa baada ya kunasa faili la wapinzani wao sasa kazi ni kujiweka sawa ili kuweza kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi.

Yanga wamefanikiwa kutuma maofisa wao nchini Algeria mapema ikiwemo kufuatilia mechi za wapinzani wao hao ambao wanatarajia kucheza mchezo wa ligi nchini humo Novemba 19 mwaka huu dhidi ya JS Kabylie.

Licha ya mtu kwenda nchini humo lakini kocha Gamondi amekuwa akiendelea kuwasoma wapinzani hao na kufanyia kazi katika mazoezi yao yanayoendelea kwenye kambi yao ya Avic Town, iliyopo Kigamboni kujiandaa na mchezo wa Novemba 24, mwaka huu, uwanja wa Stade du 5, Juillet, nchini Algeria.

Ofisa habari wa Yanga, Kamwe amesema wanafahamu ubora wa wapinzani wao na viongozi wameshafanikiwa kutimiza matakwa ya benchi la ufundi kuweza kupata baadhi ya video na kuangalia.

Amesema wamefanikisha hilo lakini pia kuna mtu kwenda nchini humo kwa ajili kuwafatilia na kwenda kuwaandalia maandalizi mazuri ya wachezaji watakapofikia.

“Kila kitu kinaenda vizuri kuelekea mchezo wetu huo dhidi ya CR Belouizdad na benchi la ufundi linaendelea kufanyia kazi bora na kukisuka kikosi kwenda kutafuta matokeo mazuri ugenini.

Licha ya wachezaji kutokamilika wote, wengine wakiwa kwenye majukumu ya timu za Taifa, lakini Kocha (Gamondi) anaendelea kuwaweka imara nyota waliopo kambini na kupitia mikanda na mechi za wapinzani wetu,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa wana kikosi bora na wachezaji wanaweza kufikia malengo yao ya kutafuta matokeo mazuri katika mchezo huo wa ugenini kuendelea walipoishia kwa kuonyesha soka safi ugenini.

“Ukiangalia rikodi za msimu uliopita mashindano ya kimataifa ugenini tumefanya vizuri, kuvuna alama moja na hata katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho tumetolewa kwa kanuni, msimu huu tunaanzia tulipoishia,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  WAKATI INONGA TAYARI AMERUDI...MBRAZILI SIMBA AAPA KUKOMAA NA KENNEDY JUMA...