Habari za Simba SC
Habari za michezo

UONGOZI SIMBA WAWAANGUKIA WACHEZAJI, ISHU IKO HIVI

Staff Desk November 17, 2023 11:45 am

Uongozi wa Simba SC umewataka Wachezaji wa Klabu hiyo kupambana na kutambua uchungu wanaoupata Mashabiki na Wanachama pale mambo yanapokwenda mrama.

Ombi hilo kwa Wachezaji wa Simba SC limewekwa hadharani kufuatia mambo kuwaendea mrama wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Young Africans, uliomalizika kwa Mnyama kupigwa 5-1, Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Novemba 05.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema wachezaji wanapaswa kutambua hilo na kuhakikisha wanapambana vilivyo katika kila mchezo ili kufanikisha furaha kwa Mashabiki na Wanachama ambao wamekuwa bega kwa bega na timu yao.

“Wachezaji sisi tuna imani nao, tarehe 25 wakaendeleze makubwa. Waamke sasa wakaipiganie Simba. Wanayo kazi kubwa ya kutufutia hizi kejeli kwa wao kufanya vizuri. Tukipata matokeo mazuri watapunguza machungu makubwa tunayopita hivi sasa.”

“Ni muhimu wajue pale hawachezi tu kwa ajili yao bali kwa ajili ya Simba. Sisi tutaenda kutimiza wajibu wa kushangilia, na wao watupe furaha ili turejeshe hali yetu ya kutamba. Tunawambia hivyo kwa niaba ya mgeni rasmi, mashabiki wa Simba.” amesema Ahmed Ally

JKT TANZANIA NA SOKO LA USAJILI DIRISHA DOGO KUELEKEA MECHI NA ASEC MIMOSAS….MASTAA NA MSHABIKI SIMBA WAPEWA UJUMBE HUU MZITO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply