Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA ASEC…MASHABIKI SIMBA WAJA NA JIPYA HILI KWA MABOSI…

KUELEKEA MECHI NA ASEC…MASHABIKI SIMBA WAJA NA JIPYA HILI KWA MABOSI…

Simba SC

BAADA ya Sintofahamu na kutokea mengi na mashabiki na wanachama kurushia maneno, uongozi wa Simba umekuja na Simba imekuja na mpango mpya kuweka karibu mashabiki kuwapa kipaumbele katika mambo mbalinbali yanahusu klabu hususani kuelekea mchezo wao wa Jumamosi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Hatua hiyo ni baada ya mashabiki na wanachama wa klabu ya Simba hivi karibuni walirushia maneno viongozi wao baada ya kufungwa mabao 5-1 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga.

Kuelekea mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Asec Mimosas viongozi wa Simba wameamua kushikamana na kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yao hususani mechi hiyo kuhakikisha Mpinzani wao hawatoki katika dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema dhumuni lao ni kuimarisha kauli mbiu yao ya Simba nguvu moja na kusahau yote yaliyopita na sasa kuweka mambo.

Amesema kuelekea mchezo wao wa jumamosi wanakuunganisha nguvu zao na wote kuwa kitu kimoja ili kufanikiwa malengo ya ya kusaka ushindi dhidi ya Asec Mimosas.

“Mchezo huu unahitaji zaidi mashabiki kuja uwanjani, tunataka kuendeleza utamaduni wa kujaza uwanja. Tumewachukua mashabiki waje kuwambia mashabiki wenzao kuja uwanjani. Hivi karibuni tumepata tuzo ya mashabiki bora Afrika kama klabu tunataka kuwashukuru kwa kazi kubwa.” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa wanahitaji kuonyesha ukubwa wao kwa kuendeleza kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa lazima waungane na mashabiki wao kuhakikisha wanamfunga Asec Mimosas uwanja wa Mkapa.

Amesema kulingana na maandalizi ya timu yao wanaimani kubwa wapinzani wao kitawakuta kile walichokipata mwaka jana walipokutana katika dimba la Benjamin Mkapa.

“Kwa umoja wetu huu, kilichowakuta mwaka jana ndio tunaenda kukifanya hicho siku ya jumamosi kumfunga Asec Mimosas hapa nyumbani, ndio kitachotea katika uwanja kwa mara nyingine,” amesema Ahmed.

Kwa upande wa Mashabiki wa Simba, akiwemo Justine Mwakitarima amewataka wanasimba wenzao kujitokeza kwa wingi uwanjani kusapoti timu yao na kuendeleza ubora wao ambao hivi karibuni Shirikisho la mpira wa miguu ulimwenguni (Fifa) walitoa tuzo bora kwa mashabiki wa Wekundu hao wa Msimbazi.

“Twendeni kwenye uwanja kwa wingi ili kuwa ni sehemu ya kuwapa hamasa wachezaji wetu kupambania klabu siku ya jumamosi dhidi ya Asec Mimosas,” amesema

Amesisitiza kuwa wanatakiwa kusahau yote yaliyopita nyuma na sasa nguvu na akili zao ni kwenda kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa ili kuonyesha kile ambacho walitunukiwa na Fifa kuwa Simba ni mashabiki bora.

Msimu uliopita Simba ilifanikiwa kuwafunga mabao 3-1 katika dimba hilo ukiwa ni mchezo wa maruadiano na kuhakikisha msimu huu kufanya vizuri zaidi kwa kuendelea walipoishia dhidi ya Asec Mimosas.

SOMA NA HII  WAKATI CHUPA YA MVINYO WA SIMBA KUHUSU MABADILIKO IKIWA INACHAKAA...CHUPA YA YANGA NDIO KWANZA MPYAAA...