Home Habari za michezo GAMONDI AMUA KUFANYA KWELI LIGI YA MABINGWA

GAMONDI AMUA KUFANYA KWELI LIGI YA MABINGWA

Habari za Yanga leo

KOCHA Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi ameanza kuwafatilia CR Belouizdad ya Algeria kuona ubora wa wachezaji wake kwa ajili ya kukabiliana katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gamondi amesema baada ya mchezo wao na Coastal Union na kuibuka na ushindi alianza kufanya maandalizi ya program ya kikosi chake kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria.

Gamondi amesema wakati baadhi  wachezaji ambao hawako kwenye majukumu ya timu za Taifa na waliobakia wakiendelea  program maalum ya kufanya kulingana na mechi yao ijayo ya kimataifa.

Amesema kazi kubwa ni kufanya tathimini ya wapinzani ambao wanakutane nao kuangalia ubora na madhaifu yao hasa wanapokuwa nyumbani.

“Kila mechi imekuwa na maandalizi yake baada ya kupata matokeo mazuri  katika michezo miwili ya ligi na sasa kuna mapumziko mafupi ya ligi kusimama na  kupisha kalenda ya FIFA kwa timu za taifa.

Wachezaji waliobaki tunaendelea na maandalizi hatutakuwa na muda kwa sababu tutaingia kujiandaa na mechi za kimataifa, sasa  tunautumia kuwafatilia CR Belouizdad katika michezo yao ya ligi,” amesema Kocha huyo.

Ameongeza kuwa anawafuatilia CR Belouizdad katika michezo yao ya ligi ambapo juzi walipoteza kwa mabao 2-1 na USM Alger, wanatarajia kucheza mechi mbili kabla ya kukutana na Yanga.

Kocha huyo amesema anawafuatilia katika michezo hiyo ambayo wanacheza lakini pia kuangalia mikanda ya video ya mechi za kimataifa ambazo wanacheza kuona jinsi ya uchezaji wao.

Gamondi amekuwa akifuatilia michezo ya wapinzani wanapokuwa wakicheza hivyo  Novemba 11 na 19, mwaka huu, atakuwa akiwafatilia CR Belouizdad ikishuka dimbani dhidi ya Paradou na JS Kabylie.

Naye Ofisa habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema uongozi pamoja na benchi la ufundi lilifanya tathimini ya wapinzani wao watakaokutana nao katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Amesema tayari kocha Gamondi ameanzq mchakato wa maandalizi ya mechi hiyo ya ligi ya Mabingwa kufatilia wapinzani wao na kulingana na jinsi ya kundi lao wanaimani kufanya vizuri.

“Tupo kundi moja na Al Ahly,  CR Belouizdad na Madeama, tumefanya tathimini ya hizi timu viwango vya timu hizo tunaimani ya kucheza robo fainali ya michuano hiyo,” amesema Kamwe.

SOMA NA HII  KWA HILI LA FEI TOTO LIPO LA KUJIFUNZA