Home Habari za michezo JAPO USHINDI NI MNONO ILA UKWELI WA LIGI KUU UPO HIVI

JAPO USHINDI NI MNONO ILA UKWELI WA LIGI KUU UPO HIVI

Habari za Yanga leo

LICHA ya kushinda bao 5-1, dhidi ya Simba, Kocha Mkuu amesema ushindi huo hauwezi kuamua kitu katika mbio za kuwania ubingwa na kutaka kushinda kila mechi zilizopo mbele yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo huo wa Kariakoo Dabi ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga. Mabao ya Aziz KI, Max Nzengeli ambaye alifunga mawili, Pacome kwa mkwaju wa penalti na Musonda Kennedy aliyefungulia pazia la mabao dakika ya tatu yametosha kuwatuliza Simba.

Bao pekee la Simba lilifungwa na Kibu Dennis  alitumia pasi ya Saido Ntibanzokiza.Baada ya Simba kunyooshwa mabao hayo matano na watani wa jadi.

Hayo alizungimxa  baada ya kukamilika kwa dakika 90, Gamondi alisema anajivunia kiwango cha wachezaji wake kwenye mchezo mkubwa wa Dabi na kupata ushindi mnono.

Alisema ushindi wa bao 5-1 mbele ya Simba ambayo ni timu kubwa ni suala la kujivunia lakini haimaanishi ndio safari ya ubingwa imeanzia hapo.

“Kipindi cha kwanza walikuwa vizuri,  dakika 45 ya kipindi cha pili niliwaeleza wachezaji wangu kucheza mpira , kuhusu ubingwa sasa ni mapema sana kuzungumzia, ushindi huu huuwezi kuamua kitu katika mbio za ubingwa.

Tunatakiwa kupambana kushinda kila mchezo iliyopo mbele yetu na sasa tunarejea katika uwanja wa mazoezi ikiwemo Gym kujiandaa na mchezo wetu ujao dhidi ya Yanga,” alisema Gamondi.

Beki wa Yanga, Dickson Job alisema  ushindi walioupata wameonyesha kuwa timu yao ni bora katika Ligi Kuu Bara na kulipa kisasi ambacho kiliwatesa kwa miaka mingi.

Alisema walihitaji alama tatu muhimu katika mchezo huo na walipabana na kufanikiwa kufikia malengo ya kuendelea kujiimarisha kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.

Alisema kitendo cha kupoteza katika mchezo wa Ngao ya jamii na wapinzani wao kutamba na bao 5-0 walizowahi kushinda nyuma ziliwatesa na wamelipa kisasi.

“Tulikuwa tunahutaji alama tatu katika mchezo huo ambazo tunaendelea kuongoza ligi na tumewaonyesha kuwa sisi ni bora zaidi yao,” alisema Job.

Naye kiungo wa timu hiyo, Maxi  Nzegeli amesema bado wana kazi kubwa ya kufanya katika michezo iliyopo mbele yao  wanashinda na kufika malengo yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Nzengeli alisema ilikuwa mechi ngumu  na presha sana na jambo kubwa wamepata matokeo mazuri sana kwa kuwafunga bao 5-1 wapinzani wao.

Alisema ushindi huo hauna maana ya kuwa wamemaliza na tayari wanakaribia kutwaa ubingwa kwa sababu bado wana michezo mingine na kutakiwa kushinda.

“Tunatakiwa kusahau haya matokeo na kuomba Mungu kusaidia kufanya vizuri katika michezo yetu ijayo kushunda, kumfunga Simba ni kuweka heshima kazi kubwa kutafuta ubingwa,” alisema Nzengeli.

Aliongeza kuwa hawezi kutoa ahadi yoyote kwa mashabiki zaidi ya kuwataka kujitokeza kwa wingi kila timu hiyo inapokwenda kwa ajili ya kusapoto kwa sababu ligi imekuwa na ushindani mkubwa.

Kwa upande wa kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliviera (Robertinho) alisema kipigo cha mabao 5-1 tulichopata kutoka kwa watani Yanga ni sehemu ya mpira.

Robertinho alisem kipindi cha pili tulipoteza umakini na kushindwa kuzuia nafasi ambazo wapinzani wetu walizitumia vizuri.

Alisem hatukuwa vizuri wakati wanapopoteza mpira na wapinzani waliweza kuwasoma na kutumia madhaifu yao kuwa faida kwao.

“Nawapongeza wapinzani kwa ushindi hatukuwa vizuri hasa kipindi cha pili lakini huu ni mpira na tunajipanga kwa mchezo ujao,” alisema Robertinho.

Aliongeza kuwa pia kukosa wachezaji muhimu ndani ya timu yake imepelekea wapinzani wake kupata ushindi mnono na sasa anajipanga kwa mchezo ujao dhidi ya Namungo FC.

SOMA NA HII  MSEMAJI SIMBA AINGIA MATATANI..."YANGA NI KAMA MAITI TU WANAKUJA TUWAKAMUE