Home Habari za michezo KIKOSI CHA YANGA KUTOKA KWA SIMBA MPAKA KWA WAGOSI

KIKOSI CHA YANGA KUTOKA KWA SIMBA MPAKA KWA WAGOSI

Habari za Yanga

Kikosi cha timu ya Yanga, leo kimeelekea jijini Tanga kwa ajili ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union utakaochezwa keshokutwa Jumatano kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Meneja wa Yanga SC, Walter Harrison, amesema hali ya timu kwa jumla ipo vizuri baada ya mchezo wa jana Jumapili dhidi ya Simba ambao tulishinda goli 5-1.

Harrison ameibainisha kwamba, wachezaji wote ni wazima, hivyo ni jukumu la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kuchagua nani atamfaa kulingana na mipango yake katika mchezo dhidi ya Coastal Union.

“Hali ya timu inaendelea vizuri, tunamshukuru Mungu baada ya mechi yetu ya jana dhidi ya Simba na ushindi mnono wa goli 5-1, kikosi kimeamka salama leo na tumefanya mazoezi asubuhi kwa ajili ya recovery kwa wale waliocheza na kwa wale ambao hawakuwa sehemu ya mchezo, tunamshukuru Mungu yamekwenda vizuri.

SOMA NA HII  KUELEKEA KARIAKOO DABI KESHO...STAA YANGA AWEKA UNAFKI PEMBENI...AMTAJA MGUNDA KWA HILI...