Home Habari za michezo KWA HILI LA CHAMA NI WAZI MAMBO SIO MAMBO MSIMU HUU

KWA HILI LA CHAMA NI WAZI MAMBO SIO MAMBO MSIMU HUU

Chama na Simba SC Msimu Huu

Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama mkali wa pasi za mwisho Novemba 8 2023 anatimiza saa 792 za kuganda bila kushangilia pasi yake ya bao wala kufunga ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ikumbukwe kwamba Oktoba 5 2023 ilikuwa ni mara ya mwisho kwa staa huyo wa Simba raia wa Zambia kufunga ndani ya ligi kwa msimu wa 2023/24.

Alifunga bao hilo kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya walipokomba pointi tatu ugenini.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tanzania Prisons 1-3 Simba. Kwenye mechi zilizofuata mwamba huyo aliganda kwa kushindwa kufunga wala kutoa pasi ya bao.

Siku 33 zimeyeyuka kwa staa huyo kushindwa kuonyesha makali yake kwenye kikosi hicho. Alikuwa shuhuda ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yanga katika Kariakoo Dabi iliyochezwa Novemba 5.

Msimu wa 2022/23 Chama alikuwa ni namba moja kwenye kutoa pasi za mwisho alipotoa pasi 14 za mabao upepo umekuwa mgumu msimu huu akiwa katoa pasi moja ya bao na kutupia mabao mawili.

SOMA NA HII  CHAMA,MUSONDA WAREJEA ZAMBIA..... ISHU IKO HIVI