Home Habari za michezo MANULA KUIKOSA ASEC KISA HIKI HAPA

MANULA KUIKOSA ASEC KISA HIKI HAPA

Simba SC inatarajiwa kumkosa Aishi Manula kwenye mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Asec Mimosas katika Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni

Kwa mujibu wa Kocha wa Simba Daniel Cadena akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo amesema Manula ana maumivu kwenye mguu wake na ataukosa mchezo huo.

Cardena pia amesema Clatous Chama amewasili jana nchini kutoka Zambia na watamtazama leo mazoezini kama yupo fiti kucheza mchezo wa kesho.

“Manula tutamkosa katika mchezo wa kesho kwakuwa ana majeraha,Clatous Chama amewasili jana akitokea Zambia,tutaona kama itawezekana kumtumia dhidi ya Asec Mimosas” amesema Cadena

SOMA NA HII  CHAMA , PHIRI WAKABIDHIWA 'HIRIZI' ZA KUWAMALIZA WAZAMBIA WENZAO...