Home Habari za michezo YANGA WASHINDWA KUTAMBA UGENINI, WAPOKEA KIPIGO KIZITO

YANGA WASHINDWA KUTAMBA UGENINI, WAPOKEA KIPIGO KIZITO

Habari za Yanga

MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameanza vibaya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-0 na wenyeji, CR Belouizdad usiku huu Uwanja wa Julai 5, 1962 Jijini Algiers nchini Algeria.

Mabao ya CR Belouizdad katika mchezo huo wa Kundi D yamefungwa na kiungo Abdelraouf Benguit dakika ya 10 na washambuliaji, Abderrahmane Meziane Bentahar dakika ya 45 na ushei na Mgambia Lamin Jallow dakika ya 90 na ushei.

Mechi nyingine ya Kundi D itachezwa kesho baina ya wenyeji, Al Ahly dhidi ya Medeama Ghana Uwanja wa Al Ahly Jijini Cairo nchini Misri.

Yanga watashuka tena dimbani Desemba 2 kumenyana na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri Uwanja wa Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam na CR Belouizdad watasafiri hadi Ghana kucheza na Medeama.

SOMA NA HII  YANGA HAINA KUPOA HAPA SANKARA, MSUVA HERSI AFANYA UNYAMA