Home Habari za michezo ZA NDAAANII KABISA…..BAADA YA KUPIGWA 5G….USAJILI MPYA SIMBA HUU HAPA….

ZA NDAAANII KABISA…..BAADA YA KUPIGWA 5G….USAJILI MPYA SIMBA HUU HAPA….

Tetesi za Usajili Simba SC

WAKATI dirisha la usajili likitarajiwa kufunguliwa Desemba mwaka huu, Kiungo wa Mtubwa Sugar na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Ladeki Chasambi ameingia kwenye orodha ya usajili ndani ya klabu ya Simba.

Taarifa za uhakika zilizoifikia jana kuwa viongozi wa klabu ya Simba wameanza usajili kuboresha kikosi chao kwa kufanya usajili ikiwemo nyota huyo kutoka kwa wakata miwa hao wa Manunngu.

Mtoa habari huyo amesema Chasambi amekuwa na mazungumzo mazuri na makubaliano ya awali yameanza kufanyika kwa nyota huyo kupewa mkataba wa awali.

“Ni kweli usajili umeanza kufanyika, Chasambi amekuwa katika mazungumzo na Simba bado yanaendelea kwa sababu wameshakubalia kwa mkataba wa awali, huu usajili utakuwa pendekezo kwa mchezaji mzawa,” amesema mtoa habari huyo.

Kwa mujibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema mapema kuzungumzia suala la usajili kipindi cha dirisha dogo hadi hapo tathimini ya kocha mkuu itakapofanyika.

“Kwa sasa hatuwezi kuongea usajili wa dirisha dogo kwa sababu wachezaji tulikuwa nao ni wazuri na suala la kuongeza nguvu kwenye kikosi kitafanyika baada ya kufanyika tathimini na benchi la ufundi kuona wapi wanatakiwa kupaboresha,” amesema Ahmed.

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Mtibwa Sugar, Swabri Aboubakar amesema yuko kwenye kikao cha bodi ya timu hiyo.

SOMA NA HII  FURAHA YA BILIONEA YAIPELEKA YANGA MAREKANI KUPIGA KAMBI...MIPANGO YOTE INAPIKWA KWA STAILI HII...