Habari za Azam
Azam FC

USAJILI DIRISHA DOGO AZAM FC SHWAAA KENYA

Staff Desk December 1, 2023 6:45 am

Inaelezwa kuwa, Azam FC inaweza kufanya usajili wa Mlinda Lango kutoka nchini Kenya na klabu ya AFC Leopards Levis Opiyo ili kuimarisha eneo lao hilo ambalo kwa sasa Ali Ahmada, Zuber Foba na Abdulai lddrisu hakuna mwenye uhakika wa namba.

Opiyo msimu uliopita akiwa na AFC Leopards, alibeba Tuzo ya Kipa Bora katika michuano ya Mozzart Bet Cup, huku kwenye Ligi Kuu ya Kenya, akishika nafasi ya pili kwa waliokusanya clean sheet nyingi akiwa nazo 16, kinara alikuwa na 17.

“Kuna taarifa kwamba baadhi ya wachezaji wa hapa Kenya wameanza kufuatiliwa zaidi na timu za Tanzania, hiyo ni baada ya Ligi ya Kenya kuanza kuoneshwa kwenye runinga ya huko Tanzania.

“Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kutakiwa na moja ya timu huko Tanzania ni Opiyo, taarifa zilizopo ni kwamba Azam FC inaweza kumsajili dirisha dogo litakapofunguliwa,” amesema mtoa taarifa hizi.

Alipotafutwa Opiyo kuzungumzia tetesi hizo, amesema: “Bado sijawa na uhakika, lakini kama ni kweli, nipo tayari kuja kucheza Tanzania kwa sababu nataka changamoto mpya baada ya kucheza sana Kenya. Kwa sasa mkataba wangu na AFC Leopards unaelekea ukingoni, utamalizika mwishoni mwa msimu huu.”

ROBERTINHO AIBUKIA YANGA AMPA GAMONDI MBINU ZA KUIUA AL AHLY AL AHLY WATUA NCHINI KUIKABILI YANGA, WAPOKELEWA NA HAPPY NATION

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply