Home Habari za michezo BAADA YA KUCHAGULIWA KUWA BOSI WA VILABU AFRIKA…MAJUKUMU YA HERSI HAYA HAPA…

BAADA YA KUCHAGULIWA KUWA BOSI WA VILABU AFRIKA…MAJUKUMU YA HERSI HAYA HAPA…

Habari za Yanga

Rais wa Yanga, Hersi Said ametangazwa na Rais wa CAF, Motsepe kuwa Mwenyektii wa Chama cha Klabu za Afrika (ACA) katika mkutano uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Marriot Mena House, Cairo Misri.

Hersi anashika nyazifa hiyo akiwa ni Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho akisaidiwa na Jessica Motaung wa Kaizer Chiefs na Paul Basset wa Akwa United.

Rais wa CAF, Motsepe alipokutana na Wenyekiti wa klabu za Afrika Oktoba 5, mwaka huu aliwaarifu kuhusu kuundwa kwa Chama hicho kitakachosaidia Soka la Afrika kupiga hatua huku malengo Mama ni kama yafuatayo ambayo Hersi atakabiliwa nayo.

1. Kulinda na kukuza maslahi ya Klabu za Soka Afrika.

2. Kuhakikisha klabu za Soka Afrika zina uwezo wa kibiashara, ushindani wa kimataifa na kuleta faida.

3. Kuhakikisha Waamuzi, kamishna wa mechi na waendeshaji VAR (Video Assistant Referee) wanaheshimiwa, wanaaminika, wanajitegemea na kwa kiwango cha kimataifa.

4. Kujenga ubia na wafadhili, sekta binafsi na Serikali kujenga viwanja vinavyoendana na viwango vya CAF na FIFA na miundombinu na vifaa vingine vya mpira wa miguu katika kila moja ya vyama 54 vya Wanachama wa CAF.

5. Kuendeleza vipaji vya vijana wa Kiafrika, akademi za Wavulana na Wasichana na kuboresha ubora wa soka la Klabu za Kiafrika kuwa za kiwango cha kimataifa.

Chama cha Klabu za Afrika kinalenga kuwaleta pamoja wadau kutoka nyanja mbalimbali za Soka barani Afrika kwa lengo tu la kukuza ushirikiano, uvumbuzi na ubora ndani ya eneo la soka la klabu za bara hili likiwa ni wazo la Rais wa CAF mwenyewe Motsepe.

SOMA NA HII  MSAIDIZI WA KOCHA WA AL AHLY APETA NAFASI YA UKOCHA SIMBA..TRY AGAIN AFUNGUKA ...