Habari za michezo

SIMBA QUEEN MGUU SAWA KAMA JESHINI NGAO YA JAMII

Staff Desk December 8, 2023 3:16 pm

Kikosi cha Simba Queens chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Mussa Hassan Mgosi kipo tayari kwa mchezo wa Ngao ya Jamii utakaokutanisha na Yanga Princess, Desemba 09 mwaka huu.

Timu nne zitashiriki michuano hiyo hatua ya Nusu Fainali mechi zitapigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi, ambapo Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL), JKT Queens wataanza kuvaana na Fountain Gate Princess saa 9:00 alasiri kabla ya saa 12:00 jioni Simba Queens kukipiga na Yanga Princess.

Kocha Mgosi amesema wachezaji wote walifanya mazoezi ya pamoja kabla ya kujiunga na timu zao za taifa na asilimia kubwa maandalizi yamekalimika.

Ameongeza hadi sasa hakuna majeruhi hata mmoja anaamini kutokana na maandalizi ya kikosi chake kitapata ushindi dhidi ya watani wao.

“Wachezaji l6 bado tunaendelea kufanya nao mazoezi Bunju lakini 12 wapo kwenye majukumu ya timu zao za taifa na wakati wanaitwa tayari tulishajiandaa wiki mbili kabla, naamini mchezo wetu utakuwa ngumu lakini naamini tutapata matokeo,” amesema Mgosi

KAMA YANGA INATAKA USHINDI LEO BASI JAMBO HILI LAZIMA WALIACHE YANGA LEO WASIPOKUWA MAKINI HILI NDIO LITAWAKUTA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply