Habari za Yanga
Habari za michezo

YANGA SASA FRESH

Staff Desk December 13, 2023 1:48 pm

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeiondolea klabu ya Yanga adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji baada ya kumlipa mchezaji Gael Bigirimana.

Bigiramana alikuwa mchezaji wa Yanga, alifungua kesi FIFA baada ya timu hiyo kushindwa kumlipa baada ya kumvunjia mkataba.

“Bigirimana alishinda kesi hiyo, na Yanga ilitakiwa kumlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo wa FIFA ulipotolewa, lakini haikutekeleza na kusababisha ifungiwe kusajili,” imeeleza taaifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)

TFF pia imeeleza kuwa imefungulia Yanga kufanya uhamisho wa ndani wa wachezaji.

Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Desemba 16 na kufungwa Januari 15.

UONGOZI SIMBA WAFURAHISHWA NA MABADILIKO HAYA YALIYOFANYWA NA BENCHIKHA KATWILA AFUNGUKA KUHUSU MCHEZO WA YANGA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply