Home Habari za michezo KUISHUHUDIA YANGA vs MADEAMA KIINGILIO NI MIGUU YAKO GSM AFANYA KWELI

KUISHUHUDIA YANGA vs MADEAMA KIINGILIO NI MIGUU YAKO GSM AFANYA KWELI

Habari za Yanga

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amesema Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ amenunua tiketi zote za mzunguko kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Medeama itakayopigwa Jumatano ijayo Uwanja wa Mkapa baada ya mechi ya awali kumalizika kwa sare ya bao 1-1 mjini Kumasi, Ghana.

Kamwe amesema siku hiyo itakuwa ni GSM Day na Mashabiki wa Yanga siku hiyo ili kumpa heshima hiyo GSM wavae jezi ya Yanga yenye nembo ya GSM.

Yanga inahitaji ushindi ili kujiweka pazuri kwenye kundi linaloongozwa na mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri wanaofuatiwa na Medeama kisha CR Belouizdad ya Algeria.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA AMWAGA SIRI NZITO...ATATUMIA MBINU HIZI KUWAANGAMIZA RIVERS