Home Habari za michezo YANGA PRINCESS SASA WATUA KENYA KWA JAMBO HILI

YANGA PRINCESS SASA WATUA KENYA KWA JAMBO HILI

SIMBA QUEENS YAIVAA YANGA PRINCESS MARCH 22 2023

BAADA ya kumaliza mshindi wa tatu kwenye michuano ya Ngao ya Jamii kwa wanawake iliyofanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na Simba Queens kuibuka mabingwa, Yanga Princess imeingia sokoni na kuitaka saini ya mshambuliaji, Janet Bundi kutoka Vihiga Queens na timu ya taifa ya Kenya.

Kwenye michuano ya ngao, Yanga haikufunga bao lolote ndani ya dakika 90 na matokeo kuamulia kwa mikwaju ya penalti tano, wakitolewa na Simba nusu fainali na kushinda mshindi wa tatu ikiifunga Fountaine Gate Princess kwa penalti 4-2.

Mwanaspoti linafahamu mchezaji huyo tayari yupo Dar na taarifa zinasema ameshasaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia wananchi hao.

Hata hivyo, Janet aliliambia Mwanaspoti tayari yuko Dar es Salaam lakini bado hajasaini mkataba kama inavyodaiwa.

“Nipo hapa Tanzania, nimekuja mara moja lakini bado sijasajiliwa na Yanga, kama ikitokea hivyo mtasikia tu,” alisema straika huyo aliyeanza kucheza ligi ya Kenya msimu huu akiwa na mabao matano kwenye mechi nane.

Straika huyo (26) anamudu kucheza nafasi zote za ushambuliaji na beki wa kulia na alikuwa sehemu ya timu ya taifa ya Kenya ya Wanawake Harambee Starlets iliyobanduliwa nje ya mashindano ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) na The Mares ya Botswana katika raundi ya mwisho. Kenya ilipoteza kwa jumla ya mabao 2-1.

Ameshinda mataji manne ya FKF-WPL akiwa na Vihiga, pia alichangia katika kushinda kombe la Cecafa katika mashindano yaliyoandaliwa nchini kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2021.

SOMA NA HII  KUHUSU KUCHELEWA KWA JEZI MPYA ZA SIMBA...ACHANA NA 'TANATALILA'...UKWELI UKO HIVI AISEE...