Msuva Algeria
Habari za michezo

ISHU YA MSUVA KUPIGWA KIBUTI NA WAARABU…UKWELI WOTE USIOSEMWA HUU HAPA…

admin December 20, 2023 8:19 pm

Rasmi klabu ya JS Kabylie ya Algeria imechana na mshambuliaji Mtanzania Simon Msuva.

Katika taarifa yake Kabylie mbali na Msuva pia imeacha na mshambuliaji mwingine mkongwe Hichem Mokhtar raia wa Taifa hilo.

Msuva aliyejiunga na klabu hiyo Agosti 27,2023 akitokea Al – Qadsiah ya Saudi Arabia hakufanikiwa kuwa mwanzo mzuti ndani ya timu hiyo kwa kukosa kuanza kwenye mechi nyingi na Waalgeria hao.

Ujio wa kocha Mreno Lui Almeida umechangia kwa kiasi kikubwa kuondoka kwa Msuva ndani ya Kybalie baada ya kocha huyo kushindwa kukubaliana na uwezo wa mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga.

Almeida amewaambia mabosi wa Kabylie kuwa anataka washambuliaji wengine wawili wenye makali zaidi tofauti na hawa ambao a emewatema.

Inaelezwa kocha huyo amewapendekeza wachezaji wawili kutoka Ureno akitaka wasajiliwe na Kabylie haraka.

KUELEKEA AFCON 2027….UWANJA WA ULAYA KUJENGWA ARUSHA….SERIKALI WATIA MGUU… BENCHIKHA:- KWA SIMBA HIII BADO SANA…NDIO KWANZAAAA ASILIMIA 70 TU YA NAVYOTAKA IWE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply