Home Habari za michezo BAADA YA KUMALIZANA NA WAGHANA JANA….GAMONDI ASHTUKIA JAMBO HILI KWA MASTAA WAKE..

BAADA YA KUMALIZANA NA WAGHANA JANA….GAMONDI ASHTUKIA JAMBO HILI KWA MASTAA WAKE..

Habari za Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema amepata mwanga na matarajio yake kuona mabadiliko makubwa hasa katika mipira iliyokufa na kona kuwa mabao.

Amesema awali mipira hiyo ilikuwa na shida kwa wachezaji wake ambapo sasa tatizo limepungua na kuamini hapo baadae litamalizika kabisa.

Kocha huyo aliyazungumza hayo baada ya mchezo dhidi ya Medeama FC ambapo waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 ukiwa ni mchez wao wa nne wa hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa juzi uwanja wa Benjamin Mkapa. Dar es Salaam.

Gamondi amesema ilikuwa nechi kubwa kwa msimu huu na wachezaji wake kupambana na kucheza soka la kuwango cha juu zaidi kwa kupigania kupata matokeo mazuri.

Kuhusu kona na mipira iliyokufa waliyopata dhidi ya Medeama na kutoweza kusaidia, amesema shida hiyo kwa sasa imeanza kupungua na anaimani hapo baada itakwisha kabisa.

“Wachezaji wamepambana tuwapongeze kwa sababu mechi haikuwa rahisi, lakini tumetawala mchezo katika kila eneo tofauti na wenzetu nadhani kuna hii ni furaha kwa mashabiki kwa ushindi huu.

“Nilipokuwa Ghana katika vyumba vya kubadilishia nguo niliwaambia wachezaji wangi kuwa tunatakiwa kushinda mechi ya marudiano na kuwataka hilo neno liwepo kwenye akili zao na kufanikiwa katika jambo hilo,” amesema Gamondi.

Alieleza kuwa licha ya kushinda bado kundi lao ni ngumu na kila mmoja anaweza kuvuka na kusonga robo fainali .

Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amefichua siri ya ushindi wao kuwa ulianza kutengeneza nchini Ghana.

Ameeleza baada ya mchezo huo walitoka sare ya bao 1-1 walipokuwa katika chumba cha kubadilishia nguo aliwaambiwa wanahitaji kushinda mechi ya marudiano na watambue kila mchezaji anajukumu la kupambania nembo ya klabu ya Yanga.

Mwamnyeto amesema walitegemea kushinda kwenye mchezo huo kwa sababu walianza maandalizi tangu wakiwa nchini Ghana, na haikuwa mechi rahisi kwani walipambana kuvuna alama tatu.

“Hakuna siri kubwa zaidi ya kocha kila mara kutukumbusha kile alichotuambia nchini Ghana mara baada ya kukamilika kwa mechi ya ugenini na kumuhitaji kila mchezaji kupambana mechi ya leo kwa sababu ilikuwa fainali yetu,” amesema Mwamnyeto.

Ameongeza kuwa wasingepata matokeo mazuri wangepoteza muelekeo wao wa kutafuta nafasi ya kwenda kucheza robo fainali katika michuano hiyo.

SOMA NA HII  KIZUMBI 'IN' YANGA ...KUPISHANA NA MUSONDA ANAYEENDA TP MAZEMBE...STAA MWINGINE HUYU HAPA..