Habari za Yanga leo
Habari za michezo

YANGA SIO KINYONGE MPAKA DODOMA …… TABORA UNITED WAJIPANGE, MASTAA HAWA WAACHWA DAR

Staff Desk December 22, 2023 12:08 pm

Msafara wa kikosi cha Yanga SC, umewasili mapema leo asubuhi jijini Dodoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tabora United.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kesho Jumamosi saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Wachezaji wote wamesafiri na timu kasoro Khalid Aucho mwenye adhabu ya kusimamishwa mechi tatu sambamba na Lomalisa Mutambala ambaye bado hajarejea kikamilifu kutokana na kuumia kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly mapema mwezi huu.

Wakati mchezo huo ukiwa ni wa raundi ya 14 katika Ligi Kuu Bara msimu huu, kwa Yanga utakuwa ni mchezo wa 11, huku kukiwa na viporo vitatu.

Katika msimamo wa ligi hiyo, Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 27 baada ya kushuka dimbani mara 10.

MABOSI SIMBA WAMPA UHURU HUU BENCHIKHA YANGA HAWATAKI UTANI HATA KIDOGO, WAAMUA KUPITA NA UPEPO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply