Home Habari za michezo MASTAA WOTE WANAOKIPIGA ULAYA KUKIWASHA ZNZ KESHO….SHOW NZIMA IKO HIVI..

MASTAA WOTE WANAOKIPIGA ULAYA KUKIWASHA ZNZ KESHO….SHOW NZIMA IKO HIVI..

Taifa Stars

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania (Kilimanjaro Stars) kimewasili salama visiwani na tayari kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanzibar Heroes ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea katika fainali za AFCON.

Kilimanjaro Stars itashuka dimbani Jumatano ya kesho kutwa katika uwanja wa Aman dhidi ya Zanzibar Heroes, ukiwa ni mchezo wa ufundi uwanja huo ambao utatumika kwa ajili ya michuano ya kombe la Mapinduzi.

Ofisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema timu ya wachezaji 25 wameingia kambini leo (jana) na kwenda visiwani humo kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki.

Amesema baada ya mchezo huo timu itaendelea kukaa kambini hadi mwisho wa mwezi huu wataenda kuweka kambini nje ya nchini (Algeria) kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya AFCON.

“Kikosi chetu kimeingia kambini na kuondoka leo (jana) kwenda Zanzibar kucheza mchezo huo wa kirafiki baada ya hapo timu inatarajia kusafiri kwenda nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya utulivu kuelekea michezo yetu ya fainali z Afcon mwakani,” amesema Ndimbo.

Kuhusu suala la mechi za kirafiki ambazo zitacheza Kilimanjaro Stars itakapokuwa, amesema bado hawajapata ratiba kamili kutoka kwa kocha, Adel Amrouch.

Kikosi cha wachezaji 25 kilichoingia kambini makipa ni Kwesi Kawawa ( Karilsud IF – Sweden), Beno Kakolanya na Yusuf Kagoma, (Singida Fountain Gate FC), Aishi Manula (Simba). Bakari Mwamnyeto , Nickson Kibabage na Dickson Job (Yanga), Lusajo Mwaikenda na Sospeter Bajana (Azam FC).

Israel Patrick. Mzamiru Yassin, Mohammed Hussein na Kibu Denis (Simba), Edwin Balua (Tanzania Prisons), Ladeki Chasambi (Mtibwa Sugar), Adam Kasa (Ifk haninge – Sweden), Zion Chebe Nditi (Alderson Town – Uingereza) na Mark John (Kingston FC – Australia).

Wengine ni Miano Danilo ( Villena CF – Spain), Adolf Bitegeko (Volsungur IF- Iceland), Robert Yohana (Fofar Athletic – Scotland, Said Hamis (Jedinstov UB – Serbia) Tarry Allarakhia (Wealdstone – Uingereza) na Simon Msuva.

SOMA NA HII  MASTAA YANGA WAPIGWA MKWARA....