Habari za Simba SC
news

KOCHA SIMBA APIGILIA MSUMARI SAKATA LA CHAMA

Staff Desk December 29, 2023 11:25 am

Kocha wa zamani wa Simba SC, Patrick Phiri raia wa Zambia amesema klabu ya Simba inapaswa sasa kufikia hatua ya kuachana kabisa na mchezaji Clatous Chota Chama, ili kulinda heshima na maslahi ya klabu.

Chama pamoja na Nassoro Kapama, walitajwa hivi karibuni kuwa na makosa ya kinidhamu na hivyo kupelekea kusimamishwa kwao klabuni.

Patrick, amesisitiza inapaswa haraka sana jambo hilo la chama liwasilishwe kwenye kamati ya nidhamu ya Simba, ambayo ipo chini ya Kamanda mstaafu wa Jeshi la Polisi, Seleman Kova, ili jambo hilo kushuhulikiwa na kupata muafaka. Kama utakumbuka kamati hii chini ya Kova, iliwahi kushuhulikia masuala tofauti ikiwemo lile la Jonas Mkude, ambae kwasasa yupo Yanga SC.

Phiri, aliongezea kwa kusema licha ya kwamba Chama ni mchezaji mzuri ila nyakati hupita, ubora huisha na kubaki uzoefu tu kiuchezaji na hivyo klabu hiyo inapaswa kufikia maamuzi magumu zaidi, kwakua pia hata suala hilo linaweza kumtoa zaidi mchezoni.

YANGA YAPEWA PACHA WA MAXI, KOCHA WAKE AWAPA ONYO MABEKI YANGA WAKOMAA NA PACHA WA NZEGELI…. ISHU IKO HIVI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply