Home Habari za michezo HAWA HAPA MASTAA 5 SIMBA WALIOKICHAFUA ‘MPAKA MAX’ KABLA YA MAPINDUZI CUP….

HAWA HAPA MASTAA 5 SIMBA WALIOKICHAFUA ‘MPAKA MAX’ KABLA YA MAPINDUZI CUP….

Habari za Simba leo

Ligi Kuu ya NBC imesimama kwa takribani wiki tatu kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoanza leo Visiwani Zanzibar.

Wakati Ligi ikiwa imesimama tayari Simba wameshacheza mechi 10 wakishinda mechi saba  sare mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Wakati wanaanza msimu walikuwa na kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ lakini hadi ligi inasimama kupisha michuano hiyo timu ipo kwenye mikono  ya kocha Abdelhak Benchikha.

Katika mechi hizo kuna wachezaji ambao wamecheza dakika nyingi kuliko wengine.

Makala hii inakuletea wachezaji watano ambao wamecheza dakika nyingi zaidi

1. Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’

Mlinzi wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ ambaye ni nahodha msaidizi ndiye amecheza dakika nyingi kuliko mchezaji yoyote.

Zimbwe Jr amecheza dakika 900 ambazo ni sawa na kucheza mechi zote 10 kwa dakika 90 bila kufanyiwa mabadiliko.

Katika michezo hiyo Zimbwe amecheza kwa uwezo mkubwa huku akisaidia kupatikana kwa mabao matatu (assist).

2. Che Fondoh Malone

Mlinzi mpya wa kati, Che Fondoh Malone anashika nafasi ya pili akiwa amecheza dakika 891.

Raia huyo wa Cameroon amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi cha Simba huku akitengeneza maelewano mazuri na mlinzi Henock Inonga.

3. Shomari Kapombe

Mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji waandamizi kikosini ambaye kiwango chake hakijawahi kuwa na shaka

Kapombe ni muhimili wa Simba upande wa kulia na amekuwa akitengeneza mabao mengi ya kufunga pamoja na nafasi kutokana na ubora wake.

Katika mechi 10 tulizocheza mpaka sasa, Kapombe amesaidia kupatikana kwa mabao matatu (assist).

4. Fabrice Ngoma

Kiungo mkabaji, Fabrice Ngoma wala haitaji maelezo mengi kuelezea uwezo wake uwanjani.

Ngoma ameingia kwenye kikosi moja kwa moja na anashika nafasi ya nne kwenye orodha ya wachezaji waliocheza dakika nyingi akiwa amecheza dakika 885.

Katika mechi hizo Ngoma amefanikiwa kufunga bao moja akiwa hatoa assist yoyote.

5. Saido Ntibazonkiza

Kiungo mshambuliaji, Saido Ntibazonkiza anakamikisha idadi ya wachezaji watano waliocheza dakika nyingi mpaka sasa ligi ikiwa imesimama.

Ntibazonkiza ambaye ni mfungaji bora wa msimu uliopita amecheza dakika akiwa amefunga mabao manne huku akisaidia kupatikana kwa jingine moja.

SOMA NA HII  WAKATI SIMBA WAKIUGULIA KIPIGO CHA JUZI...AHMED ALLY AIBUKA NA HILI LINGINE..ATUPA JIWE YANGA...