Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA WYDAD….SIMBA WAPEWA TAHADHARI….MATAJIRI WA KIARABU WAPANIA KUHARIBU….

KUELEKEA MECHI NA WYDAD….SIMBA WAPEWA TAHADHARI….MATAJIRI WA KIARABU WAPANIA KUHARIBU….

Habari za Simba

Kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, dhidi ya Wydad Casablanca, Watanzania waishio nchini Morocco, wameipa onyo kali Simba SC kwa kuitaka iongeze tahadhari kila mahali kwani matajiri wa klabu hiyo wameahidi mamilioni ya fedha ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo.

Jumamosi (Desemba 09), Simba SC itacheza dhidi ya Wydad katika mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, huku timu hizo zote zikianza vibaya hatua hiyo. Simba SC imekusanya pointi mbili, Wydad haina kitu.

Chanzo cha habari kutoka Morocco, kimeeleza kuwa, huko mambo hayaeleweki hata kidogo, kutokana na matokeo mabaya ya Wydad, ambapo mabosi wa klabu hiyo wametenga zaidi ya shilingi Bilioni 2, ili kuhakikisha timu yao inaifunga Simba SC na kufufua matumaini ya kusonga mbele.

“Nina imani Simba SC inaweza kuifunga Wydad, ila wanatakiwa kuwa makini kwani kuna uwezekano wakakutana na mambo yasiyofaa mengi ndani au hata nje ya uwanja kutokana na pesa zilizoandaliwa na matajiri wa hapa Morocco.

“Hapa watu wanaandika na wengine wanasema waziwazi kabisa kuwa, haiwezi kupita Simba SC, ili Wydad itoke kwenye mashindano haya, hivyo nina mambo hayatakuwa rahisi,” kimesema chanzo hicho.

SOMA NA HII  HUU HAPA UKWELI KUHUSU WACHEZAJI WA SIMBA NA MCHEZO WA SIMBA DAY....