Home Habari za michezo KISA KUKOSA USHINDI ….GAMONDI ‘KUWACHEZESHEA MCHAKA MBWENGO’ WAGHANA….

KISA KUKOSA USHINDI ….GAMONDI ‘KUWACHEZESHEA MCHAKA MBWENGO’ WAGHANA….

Habari za Yanga SC

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Miguel Angel Gamondi amesema kikoisi chake kitalazimika kupambana na kupata ushindi katika mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi D, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Medeama SC ya Ghana.

Young Africans itacheza mchezo huo Kesho Ijumaa (Desemba 08) katika mji wa Kumasi-Ghana, ikiwa inahitajika kupata ushindi ili kufufua matumaini ya kuwa moja ya timu mbili zitakazofuzu Hatua ya Robo Fainali, kutokea Kundi D.

Gamondi ameweka wazi mpango huo wa ushindi alipozungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari mjini Kumasi akisema: Makundi kuwa mgani “Ni lazima tushinde mechi yetu ya kesho mbele ya Medeama ili tufuzu hatua inayofuata, najua sio rahisi ila tutaweza kesho kupata alama, tumepata alama moja kwenye kundi ila timu yetu imefanya vizuri kwenye michezo iliyopita”

“Leo ndio nitajua kwenye maandalizi yetu ya mwisho nini nitaenda kufanya ila alama tatu za kesho ni lazima kwa sababu ni muhimu kwetu.”

“Tunajua kundi letu ni gumu maana lina CR Belouizdad na Al Ahly timu ambazo zina uzoefu mkubwa wa mashindano haya ya CAF Champions League, wana uwezo mkubwa wana kila kitu na uzoefu wao sio wa kulinganisha na sisi, ila niwaambie tu tunaanza hapa Medeama SC kusaka alama tatu pamoja na michezo yetu ijayo ya kundi hili na imani yangu inaniambia tutafuzu katikati yao CR Belouizdad na Al Ahly”

SOMA NA HII  YANGA vs MAMELOD NI JIWE KWA JIWE....VITA IPO KWA MASTAA HAWA....PACOME NI ZAIDI YA WOTE...