Home Habari za michezo KUMBE KWENYE KUNDI ZIMA YANGA NDIO KIBONDE

KUMBE KWENYE KUNDI ZIMA YANGA NDIO KIBONDE

Habari za Yanga

Mchambuzi nguli wa masuala ya Soka Alex Ngereza kutoka TV3 amesema kuwa Klabu ya Yanga ndiyo wanaonekana vibonde kwenye kundi lao la michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika kwa kuwa ndiyo timu pekee ambayo haina pointi mpaka sasa.

Yanga itashuka dimbani leo kutupa karata yake ya pili mbele ya Al Ahly baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya CR Belouizdad ya nchini Algeria.

Katika msimamo, Al Ahly anaongoza akiwa na alama 3 na mabao 3 ya kufunga bila bao la kufungwa, CR Belouizdad nafasi ya pili na alama 3, mabao ya kufunga manne na kufungwa mawili, Medeama nafasi ya tatu akiwa na alama 3, mabao ya kufunga mawili na kufungwa manne wakati Yanga akiwa hana alama na amefungwa mabao 3.

“Yanga ndio wanaonekana Vibonde kwenye Kundi lao kuliko hata Medeama! wamemfunga CR Belouzdad ambaye amewafunga Yanga magoli matatu kwa maana hiyo Yanga wenyewe tu ndio ambao hawana hata points moja kwahiyo ndio vibonde wa Kundi.

“Medeama wenyewe wanaamini Yanga ndio kibonde wao wanaenda kuchukua points zote sita wakati huo huo CR Belouzdad wanaamini Yanga ndio kibonde wao wanaenda kuchukua points sita wakati huo huo Al ahly wanaamini kwamba hizi timu zote wanazifunga vizuri nyumbani na ugenini.

“Tusubiri tuone ila mpaka sasa Yanga ndio pekee hawana hata point moja,” amesema Alex Ngereza.

CR Belouizdad 3-0 Yanga Al Ahly 3-0 Medeama Medeama 2-1 CR Belouizdad Yanga vs Al Ahly, nani atashinda leo?

SOMA NA HII  OHOO KUMBE SKUDU ANAJAMBO LAKE NA GAMONDI...... ISHU NZIMA IKO HIVI