Home Habari za michezo MAMBO HADHRANI HIKI NDIO KILICHOMPONZA CHAMA

MAMBO HADHRANI HIKI NDIO KILICHOMPONZA CHAMA

Habari za Simba SC

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama na mwenzake Nassor Kapama wamesimamishwa na uongozi wa timu hiyo kwa sababu za utovu wa nidhamu, kwa mujibu wa taarifailiyotolewana klabu hiyo jana Desemba 21, 2023.

Sababu za kusimamishwa kwa Chama inaelezwa kuwa ni tukio alilolifanya muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Simba na Wydad Casablanca, Desemba 19, katika uwanja wa Mkapa.

Chanzo chetu kutoka Simba kinaelezwa kuwa, kabla ya kuanza kwa mechi ya Simba dhidi ya Wydad Casablanca juzi pale Benjamin William Mkapa, wakati wa kufanya Mazoezi ya kupasha misuli (warm-up), Chama alipewa maelekezo ya program ya Mazoezi na mwalimu wa viungo Kamali.

Baada ya maelekezo hayo, Chama alionekana kutokukubaliana nayo, hivyo akaanza kurushiana maneno na kocha huyo ambaye hivi karibuni alitamvulishwa kikosini hapo akiwa pamoja na kocha mkuu, Benchikha ambapo Chama aliupiga mpira chini kuonyesha kuwa amechukizwa na kitendo hicho.

Mwalimu Selemani Matola alimfata Chama na kumtuliza aachane na hicho kinachoendelea huku beki Henock Innonga alikwenda kumtuliza Mwalimu wa Viungo kamali juu ya jambo hilo kisha baada ya mchezo kutamatika Mwalimu wa Viungo.

Mwalimu Kamali alitoa ripoti kwa kocha mkuu Abdelhak Benchikha naye Benchikha akalifikisha hilo swala kwenye uongozi wa Simba na hatimaye limetolewa maamuzi hayo ya kusimamishwa na kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu na maadili.

SOMA NA HII  JOB KUTOKA NDOTO MPAKA MAFANIKIO