Home Habari za michezo UKWELI KUHUSU KIUNGO MPYA WA YANGA HUU HAPA….ISHU YA FEI TOTO ...

UKWELI KUHUSU KIUNGO MPYA WA YANGA HUU HAPA….ISHU YA FEI TOTO YATAJWA TENA..

Habari za Yanga

UONGOZI wa Yanga umekamilisha usajili wa kiungo wa JKT FC na timu ya Taifa ya vijana Zanzibar, Shekhan Ibrahim kujiunga na kikosi cha timu kipindi cha usajili wa dirisha dogi linalotarajiwa kufunguliwa mapema mwezi huu.

Taarifa kutoka Yanga kuwa tayari wamemalizana na kiungo huyo baada ya kuridhishwa na uwezo wake na kuwafanya viongozi kuvutiwa na kumsainisha mkataba.

Mtoa habari huyo ameeleza kuwa baada ya kufanikiwa kumuuza Feisal Salum kwenda Azam FC, sasa wamefanikiwa kupata mbadala wake ambaye ni Shekhan.

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa JKU ya Visiwani Zanzibar, Shadhil khatib alisema nyota huyo kwa sasa sio mali yao baada ya kukamilisha usajili na klabu ya Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu.

Amesema kwa upande wao wamemalizana na Yanga baada ya makubaliano ya uhamisho wa kiungo huyo ambaye ukifika muda Yanga watamtambulisha.

“Ni kweli kwa sasa Shekhan sio mchezaji wetu kwa sababu amesaini mkataba wa miaka mitatu na tumeshamalizana na Yamga kuhusu uhamisho wa nyoya wetu huyo,” amesema Katibu huyo.

Shekhan ni moja ya viungo bora vinana wanachipukia kwa sasa ndani ya soka la visiwani Zanzibar, mwenye ubunifu mkubwa akiwa uwanjani na ni moja ya viungo wenye mashuti makali sana.

SOMA NA HII  YANGA YAWEKA REKODI HII YA KIPEKEE LIGI KUU