Home Habari za michezo YANGA HAWATAKI UTANI HATA KIDOGO, WAAMUA KUPITA NA UPEPO

YANGA HAWATAKI UTANI HATA KIDOGO, WAAMUA KUPITA NA UPEPO

Mabosi ya Yanga wamerudi tena kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Kitanzania, Simon Msuva wakitaka kufanya mpango wa kumsajili haraka kupitia dirisha dogo baada ya kuachana na klabu ya JS Kabylie ya Algeria.

Msuva ametemwa Kabylie sambamba na mshambuliaji mwingine mkongwe, Hichem Mokhtar kutokana na viwango vyao kutomvutia kocha Lui Almeida, raia wa Ureno.

Tangu kocha huyo atue Kybalie, Msuva alishindwa kuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza kutokana na mfumo wa Mreno huyo kumkataa hivyo kwa muda mrefu alikuwa akitokea benchini na wakati mwingine kukosekana kabisa kikosini kwa kuishia kukaa jukwaani tu kama mtazamaji.

Lakini kutemwa kwa nyota huyo za zamani wa Moro United, Yanga, Difaa El Jadida na Wydad Casablanca imekuwa ni kama kurahisishiwa kazi kwa mabosi wa Yanga waliokuwa wakiisaka saini yake tangu katika dirisha kubwa lililofungwa Agosti 31 mwaka huu kabla ya mwenyewe kuibukia JS Kabylie.

Kutokana na hali hiyo Yanga kwa mara nyingine tena imejitosa mapema kuwania saini ya Msuva haraka ikitaka kumrudisha klabuni hapo ili aje kuongeza nguvu eneo la ushambuliaji.

Habari za Msuva kuachana na Kabylie, imekuwa ni njema kwa Yanga kutokana na ukweli klabu hiyo kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kusaka mshambuliaji mwenye makali kuja kuongeza nguvu kikosi hicho kilichofunga jumla ya mabao 30 katika Ligi Kuu Bara kupitia michezo 10 tu.

Mabosi wa Yanga waaamini kuwa Msuva licha ya kutemwa na Kabylie bado ana nguvu ya kuja kufanya kitu ndani ya kikosi chao.

Mwanaspoti linafahamu, bosi mmoja mzito wa juu wa Yanga amewasiliana na Msuva akimtaka kufikiria haraka kujiunga na klabu hiyo ya zamani hiyo wakati akitafuta akili mpya.

Kabla ya kuondoka nchini, Msuva aliipa Yanga mataji kadhaa na pia kuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu misimu miwili tofauti.

SOWAH AZINGUA

Mbali na Msuva Yanga inahusishwa pia na Jonathan Sowah wa Medeama ambaye juzi aliwatibua Wanayanga kwa alichokionyesha katika mechi dhidi ya Yanga kisha kumkataa kupitia mitandao ya kijamii. Wengine ni Sankara Karamoko wa Asec Mimosas na Ranga Chivaviro wa Kaizer Chiefs ya Sauzi.

SOMA NA HII  ROBERTINHO ATAMBA KUHUSU MSIMU UJAO,... LUIS MIQUISSONE ATAJWA