Home Habari za michezo YANGA LEO WASIPOKUWA MAKINI HILI NDIO LITAWAKUTA

YANGA LEO WASIPOKUWA MAKINI HILI NDIO LITAWAKUTA

Habari za Yanga

Mchambuzi wa soka nchini Shafii Dauda amesema hana hofu na Yanga lakini wanatakiwa kuwa makini sana leo kwenye mechi yao dhidi ya Medeama huko nchini Ghana.

Shafii ametoa angalizo hilo akidai Medeama wanauhitaji pia huu mchezo wa leo.

“Sina hofu na Yanga lakini nawapa angalizo, wanaenda kukutana na timu ambayo ina matarajio makubwa, jukumu kubwa ambalo wanalo ni jinsi gani watahakikisha wanapata alama tatu.”

“Wasipokuwa na mipango thabiti pointi tatu wanaweza wakazikosa vile vile, lakini ukiniuliza kuhusu matumaini sina hofu nauachia mpira uweze kutoa majibu,” alisema Shafii.

SOMA NA HII  MASTAA HAWA YANGA WAITWA TIMU ZA TAIFA