Home Uncategorized AZAM FC YAPIGA MTU 4G

AZAM FC YAPIGA MTU 4G


TIMU ya wafanyakazi wa Azam FC imefanya kweli baada ya kuwafunza soka wafanyakazi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiwanyuka mabao 4-0.

Mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa ni maalumu kwa ajili ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

Wafanyakazi wa Azam FC walionyesha umwamba mkubwa wa kutandaza soka kwa dakika zote 90 za mchezo huo.

Mabao yaliwekwa kimiani na John Matambara, aliyefunga mabao mawili huku Victor Ndozero na Feisal wakitupia mojamoja.

Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya wafanyakazi wa Azam FC, tokea timu hiyo iundwe, na mafanikio yamekuwa makubwa sana.

Timu hiyo inatoa fursa kwa timu nyingine kuomba mechi ya kirafiki ili kuonyesha burudani.

SOMA NA HII  BEKI MATATA KUTUA MAN UNITED