Home Uncategorized SIMBA YAKIONA CHA MOTO LEO TAIFA, YAAMBULIA POINTI MOJA MBELE YA WAZEE...

SIMBA YAKIONA CHA MOTO LEO TAIFA, YAAMBULIA POINTI MOJA MBELE YA WAZEE WA KUPAPASA


LICHA ya Shiza Kichuya kuifungia Simba bao la kuongoza dakika ya 11 halikufua dafu mbele ya wazee wa kupapasa Ruvu Shooting ambao walilipinduapindua ndani ya kipindi cha kwanza.

Fully Zully Maganga alimpa tabu leo Aishi Manula kwa kumtungua kichwa kilichojaa jumlajumla ndani ya wavu na kufanya ubao usome  1-1 ilikuwa ni dakika ya 36.

Jitihada za Simba kusaka ushindi ziligonga mwamba kwa kuishia kwenye mikono ya mlinda mlango wa Ruvu Shooting, Mohamed Makaka ambaye alikuwa ni nyota mwanzo mwisho.

Manula alikuwa anakoswakoswa na Maganga ambaye alikuwa anahasira na Mnyama kwa kuwa kwenye mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 3-0.

Ushindi wa leo unaifanya Simba iambulie pointi moja mbele ya Ruvu Shooting iliyokuwa ikicheza soka la darasani.

Kibindoni Simba inajikusanyia pointi 72 ikiwa nafasi ya kwanza na mabao yake 63 huku Ruvu Shooting ikijiwekea kibindoni pointi 40 ikiwa nafasi ya 11 zote zikiwa zimecheza mechi 29.

SOMA NA HII  ISHU YA MABADILIKO, SIMBA YAKUBALI KUFUATA TARATIBU ZA SERIKALI