Home Habari za michezo KRAMO AIBUKIA BONGO…SIMBA WAKIPANGA KUTAMBULISHA VYUMA HIVI 3 VIPYA….

KRAMO AIBUKIA BONGO…SIMBA WAKIPANGA KUTAMBULISHA VYUMA HIVI 3 VIPYA….

Habari za Simba

KIUNGO wa Simba ambaye ni majeruhi ya muda mrefu, Aubin Kramo amerejea nchini akiwa fiti na kujiunga moja kwa moja na kikosi cha timu kilichopo Zanzibar kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi, huku klabu hiyo pia ikitarajia kutambulisha nyota wapya watatu ndani ya wiki hii.

Kiungo wa Simba majeruhi ya muda mrefu amerejea nchini akiwa fiti na kujiunga moja kwa moja na timu kilichopo Zanzibar katika Mapinduzi huku wakitarqtajia kutbulisja nyota wapya watatu ndani ya wiki hii.

Mbali Kramo pia kuna myota mpya ametua nchini jana usiku na leo kuelekea visiwani Zanzibar kuungana na kikosi cha Simba kilichopo Visiwani humo katika mashindano ya Mapinduzi yanayoendelea.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema Kramo ametua nchini na kujiunga na timu akiwa chini ya uangalizi wa Madaktari wa timu.

Amesema kabla hajatua nchini alikuwa akifanya mazoezi mepesi na sasa Madaktari kwa ajili ya kumuangalia kisha kutoa taarifa juu ya kuwa tayari kucheza mechi za ushindani au bado anatakiwa kupewa muda zaidi.

Kuhusu usajili wa dirisha dogo, Ahmed alisema “baada ya kumtambulisha kiungo Salehe Karabaka kutoka JKU FC, ni kama rasha rasha kwenye mvua kuna usajili mkubwa unaendelea kufanyika usiopungua wachezaji watatu.

Mashabiki wa Simba wanatakiwa kuwa na subira kwa sababu viongozi wanaendelea na mchakato wote wa usajili kulingana na mahitaji ya benchi la ufundi na tunatarajia kushusha vifaa vipya,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  FADLU BADO ANALISUKA JESHI LA SIMBA...MSIKIE MOGELLA.