Habari za Michezo leo
Habari za michezo

WAKATI YANGA WAKIIKIMBIA SIMBA JANA…SINGIDA WAWAHI SITI YA MBELE KABISA…

admin January 8, 2024 8:14 pm

Singida Fountain Gate imetangulia hatua ya nusu fainali baada ya kuishangaza Azam FC kwa kuichapa mabao 2-1.

Mchezo huo wa robo fainali ya Kombe la Mapinduzi uliopigwa leo Jumatatu kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Singida FG ilitumia dakika tano tu ndani ya kipindi cha pili kutengeneza ushindi kwa kusawazisha na kuongeza bao la ushindi.

Singida FG sasa inasubiri mshindi wa mechi ya Simba SC dhidi ya Jamhuri unaopigwa saa 2:15 usiku.

Azam ndio ilikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza likifungwa na mshambuliaji wake, Allasane Diao katika dakika ya pili ndani ya tano za nyongeza kumaliza kipindi cha kwanza, akifunga kwa kichwa akimalizia kros ya beki wake wa kushoto Pascal Msindo.

Bao hilo ni la nne kwa Diao kwenye mashindano haya ya msimu huu ya Mapinduzi akiwa mmoja wa vinara wa ufungaji akiendeleza moto wake kwenye mashindano hayo.

Bao hilo likazifanya timu hizo kwenda mapumziko huku Azam ikiongoza 1-0 huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.

Kipindi cha pili Singida ikarudi na nguvu kubwa ikisaka bao la kusawazisha na juhudi zikalipa dakika ya 61 ikipata bao mfungaji akiwa mshambuliaji Elvis Rupia akimalizia kwa kichwa krosi ya mshambuliaji mwenzake Habib Kyombo.

Wakati Azam ikijipanga kusawazisha ikajikuta inapigwa bao la pili kwa shambulizi la haraka dakika ya 65 mfungaji akiwa Kyombo akimalizia kwa kichwa mpira wa Rupia akilipa fadhila kwa kumtengenezea krosi nzuri mfungaji.

Mpaka mwisho wa mchezo Singida ikafanikiwa kukata tiketi ya kucheza nusu fainali kwa mara ya pili mfululizo ikisubiri mshindi kwenye mchezo wa baadaye usiku kati ya Simba dhidi ya Jamhuri.

KWA HALI HII YA CHAMA NA BENCHIKHA….NI ZAMU YAKE KWENDA YANGA SASA… WAKATI JAMBO LA CHAMA LIKIWA TETE….BENCHIKHA AMPIGA MKWARA MZITO PHIRI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply