Home Habari za michezo PENATI YA KAGERE NA UTAMU WA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA….UKWELI UKO...

PENATI YA KAGERE NA UTAMU WA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA….UKWELI UKO HAPA

Habari za Simba leo

Ni kweli mechi ya nusu Fainali Mapinduzi ilikuwa ni Singida na Simba. Lakini inakuwa mechi kubwa na inazungumzwa vya kutosha Kwa kuwa tu inahusika Simba na ikihusika Simba lazima na Yanga waitolee macho.

Mashabiki wa Yanga Wana uwezo mkubwa Sana wa kuzusha mambo na wakayapigia kelele mpaka yakaonekana ni agenda.
Hata wachambuzi wa vipindi vya michezo katika vyombo vya habari Leo nao wamegawanyika.

Wapo wa upande wa kuiponda Simba na wapo walio upande wa Simba. Ilimradi tu ukiwasikiliza utagundua huyu ana maumivu makali moyoni na huyu ni burudani Kwa kwenda mbele.

UHALISIA UPOJE?

Nani hakuona Singida walivyokuwa wanapoteza muda uwanjani? Mara ngapi kipa alijilaza? Mpira unapigwa unagonga mwamba kipa anajilaza dakika mbili.

Mwamuzi anaonyesha muda wa kufidia muda uliopotea bado wanapoteza muda. Kibaya zaidi wanalala kisha wanamzuia daktari asiingie uwanjani Ili muda uendelee kupotea. Na kama ulikuwa makini kama Mimi utakuwa uliona refa akiwaonyesha ishara nyie potezeni muda Mimi ninatumia saa yangu.

Refa aliongeza dakika sita. Akaamua kufidia muda walipoteza. Kabla ya muda huo kumalizika inapatikana Kona. Mlitaka kona isipigwe? Kona lazima ipigwe.

JE ILIKUWA KONA KWELI?

Karudie tena kutazama. Wakati Saidoo anapiga mpira. Kelvin Kijiri aliugusa? Ni wazi aliugusa.

Umejuliza muda ule mpira unakwenda nje. Ambapo kitendo Cha mpira kwenda nje ni ahueni zaidi ya muda kupotea zaidi. Kwa nini kipa Parapanda anahangaika kuudaka mpira ambao unakwenda nje iwe golikiki? Ni wazi anajua huu mpira ukienda nje ni Kona. Hivyo anahangaika kuudaka Ili kunusuru Simba wasipate Kona.

Umejiuliza hivi ingetokea Che Malon ndio angeokoa mpira Kwa mkono kama alivyofanya Mangalo. Leo mitandao ingekuwaje? Wachambuzi uchwara Leo wangeamka na misemo mingapi kuhusu hilo? Tazama Leo umeona linasemwa?

*Makala haya yameandikwa na kusambazwa na shabiki wa soka nchini ndugu Mgalilaya*.

( Jicho la tatu la Mgalilaya).

SOMA NA HII  WAKATI YANGA NA GSM WAKITAKA KUMPA MIL 400 ...HIVI NDIVYO MO DEWJI ALIVYOFANYA KUFURU ISHU YA CHAMA....