Home Habari za michezo PACOME AJITISHWA ‘ZIGO’ LA LIGI YA MABINGWA KWA YANGA…

PACOME AJITISHWA ‘ZIGO’ LA LIGI YA MABINGWA KWA YANGA…

Habari za Yanga leo

KIUNGO Mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua ameweka wazi kuipigania timu yao haswa katika michuano ya kimataifa ili waweze kuvuka hatua waliyopo na kwenda katika hatua ya robo fainali.

Pacome ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu hu anashika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora akiwa na mabao matatu, bao moja nyuma ya kinara anayeongoza ambaye ni Sankara Karamoko wa Asec Mimosas.

Pacome alisema kuwa wanatambua umhimu wa kuvuka hatua hiyo ya makundi na kwenda hatua ya robo fainali kwani kwa ukubwa wa timu hiyo kwa sasa wanatakiwa kuwa na uhakika wa kufikia hatua hiyo.

โ€œTunafahamu kuwa Yanga ni timu kubwa na katika michuano hii tunatakiwa kuhakikisha kuwa tunaivuka hii hatua na kuwez akutinga katika hatua inayofuata mabayo ni hatua ya robo fainali.

โ€œSio rahisi lakini tunaweza kufika kwa kuwa kila mchezaji wa Yanga anatamani na tumeongea tumekubaliana tuweze kufikia malengo yetu hivyo tutaipambania timu kufikia huko,โ€ alisema Pacome.

SOMA NA HII  BAADA YA UKIMYA MREFU....HATMA YA NKANE YANGA YATUPWA KWA NABI...ISHU NZIMA IKO HIVI...