Habari za Yanga leo
Habari za michezo

YANGA WAUSHIKIA BANGO UBINGWA WA MLANDEGE….ALLY KAMWE ATUPA DONGO GIZANI…

admin January 15, 2024 1:30 pm

ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa alitabiri tangu awali kuwa Mlandege walikuwa na nafasi ya kutwaa taji la Mapinduzi 2024 kwa mara nyingine tena.

Ipo wazi kuwa Januari 13,2024 ubao wa Uwanja wa New Amaan Complex ilikuwa Mlandege 1-0 Simba na taji likabaki Zanzibar.

Bao pekee la ushindi lilipachikwa dakika ya 54 na Joseph Akandwanao aliyewavuruga Simba kwenye mchezo huo kwa bao hilo lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.

Kamwe baada ya Yanga kuondolewa hatua ya robo fainali na APR alisema: “Nimewaona Mlandege ni timu nzuri na wachezaji wanajituma hakuna timu inayoweza kuizuia kutwaa ubingwa hivyo nina amini itakuwa hivyo,”.

Baada ya Mlandege kutwaa ubingwa Kamwe amesema:”Nilishasema kwa kuwa naujua mpira na imekuwa hivyo,”.

YANGA KUMALIZA USAJILI NA MASHINE HII YA HATARI….JAMAA NI MAYELE MTUPUU… BAADA YA KUGOTESHWA KWENYE MAPINDUZI CUP….GAMONDI AAPA KUFA NA HILI NDANI YA YANGA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply