Usajili Mpya Simba leo
Habari za michezo

SAPRAIZI YA MWISHO SIMBA HII HAPA…..MASHINE YA KAZI KUTAMBULISHWA…YANGA WALIMTAKA…

admin January 16, 2024 5:08 pm

Simba wakati wowote itamtambulisha rasmi winga mpya Edwin Balua baada ya kumalizana naye kila kitu.

Awali usajili huo ulikaribia kuingia mwiba baada ya watani wao Yanga kugundua kwamba pande hizo mbili kati ya Simba na Prisons bado hawajamalizana masuala ya fedha hali ambayo iliweka njia panda ukamilifu wa dili hilo.

Hata hivyo Simba iliwahi kuweka ‘mzigo’ kwa Prisons na kumaliza utata huo akisalia mchezaji pekee kwenda kumalizia masuala ya mwisho ya utambulisho.

Wakati wowote kuanzia sasa Simba itamtambulisha rasmi Balua kuwa winga wao mpya kwenye kikosi chao akiwa ni mchezaji wa mwisho kutambulishwa kwenye usajili wa dirisha dogo.

Simba tayari imeingiza kwenye mfumo wa usajili jina la Balua kwenye dirisha la usajili lililofungwa usiku wa kuamkia Leo.

Balua anakuwa mchezaji wa sita kusajiliwa na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo wengine ni Babacar Sarr, Ladack Chasambi, Saleh Karabaka na washambuliaji Pa Omar Jobe na Freddy Kouablan

USAJILI WOTE ULIOKAMALIKA BONGO HUU HAPA….ISHU YA BALEKE NA PHIRI BADO NGUMU… UKWELI KUHUSU ‘MZUNGU’ ANAYECHEZA TAIFA STARS….ASILI YAKE NA JINSI ALIVYOPEWA SHAVU LA AFCON…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply