Home Habari za michezo WAKATI WAKITENGA BIL 25…, HIVI NDIVYO SIMBA WALITUMIA BIL 15 KUSHINDA NGAO...

WAKATI WAKITENGA BIL 25…, HIVI NDIVYO SIMBA WALITUMIA BIL 15 KUSHINDA NGAO ZA JAMII TU…

Habari za Simba leo

UONGOZI wa Simba hatimaye umeweka wazi bajeti ya msimu mpya wa fedha wa klabu hiyo wa mwaka 2023/24 wakiwa na malengo ya kuweza kukusanya jumla ya Shilingi Bilioni 25 kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato.

Huku wakitangaza faida ya bilioni 3 waliyoipata kutoka kwenye bajeti ya msimu wa fedha wa mwaka 2022/23 baada ya kukusanya Bilioni 15.9 huku awali wakiwa waliweka malengo ya kukusanya Bilioni 12.3.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Simba Mhasibu wa Klabu Suleiman Kahumbu alisema kuwa “”Matumizi ya 2022/23 yalipangwa kuwa Tsh. 12,363,626,983 lakini matumizi halisi ni Tsh. 15,936,829,943. Bajeti kwa mwaka 2023/2024 klabu imepanga kukusanya kiasi cha Tsh. 25,930,722,300 lakini imepanga kutumia kiasi cha Tsh. 25,423,997,354. Tutabaki na mapato ya ziada ya Tsh. 506,724,946.”- Mhasibu wa Klabu, Suleiman Kahumbu.

“Aidha mapato yote hayo yanapatikana kutokana na vyanzo mbalimbali vya mapato ndani ya timu hiyo kama fedha ya mdhamini,Hakiza matangazo,Mapato ya Mlangoni,uuzwaji wa jezi.wadhamini wadogo wadogo na kushiriki katika michuano ya AFL ajmbo ambalo limechangia kwa asilimia kubwa kuweza kupata mapato makubwa kwa klabu yetu msimu huu.

MO DEWJI ACHANGIA BILIONI 2.4
“Katika bajeti ya fedha ya msimu wa 2022/23 rais wa heshima wa Simba Mohamed Deji alituchangia kiasi cha shilingi bilioni 2.4 ambazo zilienda moja kwa moja kwenye kufanikisha kukusanya Bilioni 15 ambazo zimetupa faida kwa kiasi kikubwa.

USAJILI WATUMIA BILIONI 2,387
“Kwenye usajili ambao tumeufanya msimu wa 2022/23 tuliweza kutumia kiasi cha shilingi bilioni 2.3 ambapo ni kwa wale wachezaji wapya ambao tuliweza kuwasajili kwa wale wa kimataifa kwa manaa ya wachezaji wa nje na wandani.

MISHAHARA WATUMIA 4,889
“Mishahara wa wachezaji imeweza kutugharimu zaidi ya shilingi bilioni 4.8,ikiwa ni bajeti ya msimu wetu wa fedha kwa mwaka 2022/23 hapa utaona ni kwa kiasi gani tunaweza kutumia fedha nzuri kuwalipa wachezaji wetu stahiki zao.

BONASI ZA WACHEZAJI 1,5
“kwenye michezo ambayo Simba inakuwa inacheza basi kuna bonasi kwaajili ya timu na hapa inakuwa kwa upande wa timu zote ile ya kijme na ile ya kike Simba Queens,” alisema Suleima Kahumbu,Mhasibu wa Simba.

Katika mkutano huo ulianza aaa 5:00 asubuhi uliofunguliwa na Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu alisema Simba imeshafanya mambo mengi makubwa, yaliyopita, yanayofanyika sasa na mengine yanakuja.

Alisema viongozi wenye dhamana ya kuongeza klabu hiyo wapo tayari kupokea maoni na kukosolewa ili kuipeleka Simba mbele na kufikia malengo yanayotarajiwa.

“Lengo letu ni kujenga umoja. Mfano mtu anasema uwekezaji hauna faida wakati kabla ya uwekezaji mapato yalikuwa Tsh. 1.6 bilioni, mara baada ya uwekezaji yamepanda hadi Tsh. 6.9 bilioni.

Afrika tulikuwa nafasi zaidi ya 80 kwenye ubora na sasa tupo nafasi ya saba. Tunataka ukosoaji wenye tija, Kama mnakumbuka mlichanga pesa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja, pesa ile ilitumika kujenga ukuta wa uwanja wa Bunju na pesa zingine zilitumika kuimarisha kambi ya timu,” alisema Mangungu.

Alieleza kuwa wanajenga Simba imara kwa kizazi cha sas na baadae, kuendelea kuonyesha kushirikiana na anaimani watafanikiwa na kufikia kule ambacho kinatararajiwa na wanachama wa klabu hiyo.

Kwa upande wa mwakilishi wa mgeni rasmi, Nicolas Mihayo akimwakilisha Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo nchini (BMT), alisema anawapongeza Simba kwa kufuata malekezo ambayo ilipewa kufanyia kazi katika mapendekezo ya marekenisho ya katiba.

“ Hili ni jambo la mfano kwa timu zingine, kuzingatia yale yanayoagizwa na Serikali, ambapo hivi karibuni Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Damas Ndumbaro aliwaita Simba na kuwataka kufanyia kazi mambo kadhaa ya katika yao na inawapongeza na inawatakia kila la kheri,” alisema Mihayo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Simba, Jaji mstaafu Thomas Mihayo, aliwataka viongozi kuwasikiliza wanachama wao na kuyafanyia kazi ili kuifanya klabu hiyo inakuwa imara.

Alisema kulingana na mkutano huo viongozi na wanachama kutorubusu migogori ambayo inaenda kuathiri timu yao kwa kupata matokeo mabaya katika michezo ambapo ni toafuti na timu zingine ambazo wanakuwa na migogoro na kuathuri wachezaji.

“Kutofautiana ni jambo la kawaida, jambo la msingi ni namna gani ya kutatua maana kuna mengine yanaweza kuwa kweli na mengine sio kweli na zikitokea tofauti zisiingie kwenye timu. Mtu yoyote asiyeitakia mema Simba huyo ni msaliti.” Mwenyekiti huyo wa baraza la Ushauri Simba.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula aliweka wazi malengo ya klabu ni kujenga timu imara yenye uwezo wa kushinda makombe, kujenga taasisi imara na endelevu ikiwemo kujenga chapa imara ndani na nje ya Tanzania.

“Kujenga misingi imara na yenye tija kwa wanachama na wapenzi, kujenga uwezo wa kifedha ili kufikia malengo, kuvutia wafanyakazi wenye weredi, kujenga misingi imara ya mawasiliano na matawi/wanachama.

Tumefanya maboresho makubwa kwenye benchi la ufundi tukianzia na kocha nadhani wote mnaona, idara ya afya ya timu yetu, tuna madaktari bora sana.

Lakini pia tumeimarisha timu ya vijana kwa kutafuta vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini, timu yetu ya wanawake imekuwa bora sana. Eneo lingine ni tumeimarisha uhusiano kwa kiasi kikubwa na wadhamini wetu.

Sehemu nyingine kubwa ni kushinda Ngao ya Jamii mbili kwa timu yetu ya wanaume na wanawake kuwa mashabiki bora wa AFL. Simba ilileta Rais wa FIFA na kubwa zaidi kuitangaza Tanzania Kajula.

Aliongeza kuwa wanataka kuwa mabingwa wa ndani na nje ya uwanja, walianzisha WhatsApp channel wakawa wanasemwa lakini leo wanaongoza kuwa namba moja Afrika Mashariki na Kati.

“Tutaendelea kujenga rasilimali za Simba na eneo lingine ni kuwa na wafanyakazi wenye weledi na uwezo mkubwa sana. Mbele tunaangalia kuboresha mapato, kuimarisha biashara ya jezi.

Sandaland amefanya yale mliyokuwa mnayataka kama jezi kutoka mapema na jezi yenye ubora, mzabuni aliyetimiza malengo yenu wanachama, Mwaka huu tunaangalia namna ya kushirikisha matawi katika uuzaji wa jezi ili kuwaongezea mapato,” alisema Kajula.

Alieleza kuwa changamoto zilizopo upande wao ni rasilimali fedha kuongezeka kwa gharama za uendeshaji, kutanuka kwa mahitaji , kuumia kwa wachezaji, mabadiliko na ushindani kuongezeka na kuendelea kuwa timu namba moja.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIJIUMAUMA KWA NABI....SIMBA WAPANGA KUIFANYIA 'JAMBO BAYA' AZAM FC..