Home Habari za michezo ‘VIBE’ LA MASHABIKI YANGA LAWAKUNA MASTAA AFRIKA….TAZAMA WALICHOSEMA…

‘VIBE’ LA MASHABIKI YANGA LAWAKUNA MASTAA AFRIKA….TAZAMA WALICHOSEMA…

Habari za Yanga SC

Wakati Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Gamondi, akitarajia kubadilisha programu ya mazoezi wiki hii kutoka ya ufukweni na kurejea Uwanjani, wachezaji wa timu hiyo wamesema wamemisi sana shangwe, kelele na furaha za mashabiki wao.

Wakizungumza jijini Dar es Salaam, wachezaji Clement Mzize na Maxi Nzengeli wamesema tangu mechi za Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa na kumaliza Kombe la Mapinduzi na kuwa kwenye mapumziko, wamepooza na wameanza kuwakumbuka tena mashabiki ambao huwafuata popote waendapo, wakiwaahidi makubwa zaidi watakaporejea uwanjani.

Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa kwa sasa imesimama kupisha Fainali za Mataifa ya Bara la Afrika ‘AFCON 2023’ zinazoendelea nchini Ivory Coast.

Tumewamisi mashabiki wetu, wao hutufuata popote tuendapo, wanatushangilia kwa nguvu zote na kutupa morali, furaha na kujituma kuipambania nembo ya klabu, leo hii hatuwaoni kwa sababu mechi zimesimama na sisi tulipata mapumziko kidogo, nina imani tutakutana tena na tutakuwa na wakati mzuri kwa mara nyingine,” amesema kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli raia wa Jamhuri ya Kidemkokrasi ya Congo.

Naye Mshambuliaji Clement Mzize amesema ana hamu tena ya kuwaona mashabiki uwanjani na anajua pia hata wanachama na mashabiki wao pia wana hamu ya kuwaona wachezaji wao.

“Wananchi, wanachama na mashabiki wa Young Africans, wana hamu ya kutuona tukicheza na kupambana Uwanjani, ‘wametumiss na tumewamiss’ sana mashabiki wetu, tulikuwa nao pamoja, tuliwapa furaha na kushangilia kwa pamoja, naamini tutakuja kivingine tena, yale yamepita, tutakuja mara mbili zaidi ya mwanzo, ameahidi Mzize.

Wakati huo huo, kocha Gamondi ambaye wiki nzima alikuwa akiwafua wachezaji wake kwenye fukwe za Coco na kuwapeleka gym, anatarajia kubadilisha programu na kuhamia Uwanjani.

Meneja wa timu hiyo Walter Harrison, alisema mabadiliko hayo ya benchi la ufundi yatafanyika baada ya kuridhishwa na mazoezi ya awali waliyowapatia wachezaji.

SOMA NA HII  UBINGWA MSIMU HUU UTAENDA KWA MOJA YA TIMU HIZI 4....YANGA MHHHH!!!