Habari za michezo

BAADA YA KURUDI BONGO TENA….FAILI LA DAVID MOLINGA LATUPWA KWA MZAMBIA…NI KUSUKA AU KUNYOA….

admin August 2, 2022 2:32 am


Ameachwa? Hapana! Hatma ya straika wa Namungo aliyewahi kung’ara na Yanga misimu miwili iliyopita, David Molinga, ipo mikononi mwa kocha Mzambia Honour Janza aliyepewa faili la mchezaji huyo ili kuamua abaki kikosini au atemwe kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na ASFC.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo zinaeleza Janza ndiye anayepaswa kutoa uamuzi wa mwishokwa Molinga, kwani mkataba aliosaini Agosti 31 mwaka jana umebaki mwezi mmoja kufikia tamati.

“Jambo ambalo linasubiriwa ni kuona orodha kamili ya wachezaji wapya waliosajiliwa na baada ya hapo ndipo kocha ataamua mwenyewe kama anamuhitaji kubaki nae au amfungulie milango ya kutokea,” kilisema chanzo chetu.

Molinga amekuwa kwenye sintofahamu ya mara kwa mara katika kikosi hicho huku ikielezwa kutohudhuria mazoezi kwa wakati hali ambayo inatishia nafasi yake ya kubaki kutokana na tabia ambazo viongozi wake hawaridhishwi.

Usajili wa mshambuliaji, Matteo Anthony kutoka KMC huenda ukazidi kuweka nafasi yake finyu kutokana na uwepo pia wa nyota, Reliants Lusajo ingawa kuondoka kwa Obrey Chirwa aliyejiunga na Ihefu kunaweza kuwafikirisha mabosi wake.

Nyota huyo wa zamani wa Yanga alijiunga na Namungo baada ya kumalizana na timu ya Zesco United inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia.

KUHUSU ISHU YA AZAM KUMWAGANA NA MUDATHIRI YAHYA…UKWELI WOTE HUU HAPA…MAMBO NI KIMYA KIMYA AISEE… PAMOJA NA KUCHAPWA MPAKA AKACHAKAA JUZI…MANDONGA AMTAKA DULLAH MBABE…AMTOLEA MANENO YA ‘SHOMBO’…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply